Wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu kutanuka kutibiwa JKCI



Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifanya upasuaji kwa njia ya tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab   kumzibua mgonjwa mshipa wa damu wa moyo ulioziba.

*****************************************************************************************************************************************************************************************************************************

TAARIFA KWA WATAALAMU WA AFYA NCHINI

KAMBI MAALUMU YA MATIBABU YA MAGONJWA YA MISHIPA YA DAMU YA MIGUU KUTANUKA (VARICOSE VEIN)

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalamu wa afya nchini  kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu kutanuka kwenye miguu kwa jina la kitaalamu Varicose Vein waje kutibiwa katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya kutanuka kwa mishipa hiyo.

Matibabu hayo yatakayotolewa tarehe 12 hadi 15 Februari 2025 yatafanywa na  wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya  Andalusia ya nchini Misri.

Matibabu yatakayofanyika katika kambi hiyo ni ya upasuaji kwa njia ya kutumia matundu madogo katika kutibu mishipa ya damu ya vein iliyotanuka kwa kutumia kifaa cha umeme kijulikanacho kwa jina la laser ablation machine. 

Aidha tunawaomba wagonjwa wenye matatizo ya vidonda vya miguu visivyopona kwa muda mrefu, matatizo ya mishipa ya damu miguuni kutanuka, ganzi ya miguu na mabadiliko ya rangi miguunii wafike katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upanga kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0716-696217 Dkt. Alex Joseph, 0716162295 Dkt. Alex Msoka  na 0788-308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete .

 “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa