Tanzania Kushirikiana na Burkina Faso matibabu ya moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akiwaonesha shelfu linalotumika kuwafundisha wagonjwa kwa
vitendo namna ya kuandaa mlo kamili ujumbe wa wataalamu wa afya na washauri wa
Rais wa Burkina Faso walipotembelea taasisi hiyo jana kwaajili ya kujifunza na
kuona namna ambavyo watashirikiana katika mafunzo na matibabu ya magonjwa ya
moyo.
Afisa Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eliamini
Msangi akiwaonesha namna ya kupata huduma ya matibabu kwa njio mtandao ujumbe
wa wataalamu wa afya na washauri wa Rais wa Burkina Faso walipotembelea taasisi
hiyo jana kwaajili ya kujifunza na kuona namna ambavyo watashirikiana katika
mafunzo na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwaonesha moja ya chumba cha VIP ujumbe wa wataalamu wa afya na washauri wa Rais wa Burkina Faso walipotembelea taasisi hiyo jana kwaajili ya kujifunza na kuona namna ambavyo watashirikiana katika mafunzo na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Alex Benjamini akiwaelezea huduma zinazotolewa katika chumba cha
upasuaji ujumbe wa wataalamu wa afya na washauri wa Rais wa Burkina Faso walipotembelea
taasisi hiyo jana kwaajili ya kujifunza na kuona namna ambavyo watashirikiana
katika mafunzo na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Daktari bingwa wa Upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiwaeleza namna wanavyochagua watoto
wakufanyiwa upasuaji wa moyo ujumbe wa wataalamu wa afya na washauri wa Rais wa
Burkina Faso walipotembelea taasisi hiyo jana kwaajili ya kujifunza na kuona
namna ambavyo watashirikiana katika mafunzo na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi mshauri wa Rais wa Burkina Faso katika
masuala ya Rushwa Ragnang-newinde Isidore walipotembelea taasisi hiyo jana kwaajili
ya kujifunza na kuona namna ambavyo watashirikiana katika mafunzo na matibabu
ya magonjwa ya moyo.
*********************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kushirikiana na nchi ya
Burkina Faso kuwajengea ujuzi wa ubingwa bobezi wa matibabu ya moyo wataalamu
wa afya wa nchi hiyo.
Hayo yamesema na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge baada ya kukutana na ujumbe wa
wataalamu wa afya na washauri wa Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore
jana Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kisenge alisema Rais wa Burkina Faso baada ya kuona maendeleo
makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo akaamua kutuma ujumbe huo ili waweze kuona
na wao waende kuanzisha taasisi kama hiyo.
“Taasisi hii ni moja ya taasisi kubwa barani Afrika kutoa na huduma
za matibabu bobezi ya moyo tunayoyatoa, Burkina Faso wameamua kuitumia taasisi hii
kuwakuza kama ambavyo Rais wao amekuwa akisema maendeleo ya Afrika yatajengwa
na waafrika wenyewe”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema baada ya kuzungumza na ujumbe huo wamekubali
kuleta wataalamu wao kujifunza JKCI, kuleta wagonjwa ambao walikuwa wakiwapeleka
nchi za Ufaransa na Uturuki kwani maendeleo yaliyopo JKCI ni makubwa hivyo
hawaoni sababu ya kuendelea kuwapeleka nje ya Bara la Afrika.
“JKCI tutashirikiana na Burkina Faso kwa kuwapeleka wataalamu
wetu kubadilishana nao ujuzi, kufanya tafiti kwa pamoja, kuwaongoza katika
manunuzi ya vifaa tiba kupitia Bohari yetu ya Dawa (MSD) hivyo kuongeza kipato
cha nchi yetu”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka
nchini Burkina Faso Adam SAWADOGO alisema baada ya kuona Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete kuwa moja ya Taasisi zinazoongoza Barani Afrika kutoa huduma za
kibingwa bobezi Rais wa Burkina Faso akawatuma kufika na kujionea ili waweze
kuiga na kuboresha huduma za matibabu ya moyo nchini humo.
“Baada ya kufanya ziara katika Taasisi hii tumeona inakidhi
viwango vya kimataifa, kama waafrika tunajivunia kufanya kazi na ninyi na
mtakuwa ndio washirika wetu wakuu katika kufikia malengo yetu ya kuwa na
Hospitali ya ubingwa bobezi wa magonjwa ya moyo”, alisema Dkt. Adam
Dkt. Adam alisema kwa niaba ya Rais wa Burkina Faso Kapteni
Ibrahimu Traore na wanachini wake wanaushukuru uongozi wa Tanzania kwa
kuwapokea na kukubali kuwasaidia kufikia malengo ya kuanzisha Hospitali ya
moyo.
Naye Mratibu wa Utalii Matibabu kutoka Wizara ya Afya Dkt.
Asha Mahita alisema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwenye masuala ya afya
iliyopelekea kupata tuzo ya The Gates Goalkeepers Award kama kielelezo cha
matokeo makubwa yaliyopatikana kufuatia ripoti ya afya ya mwaka 2022.
Dkt Asha alisema kutokana na changamoto walizonazo Burkina
Faso katika masuala ya matibabu ya moyo imepelekea kutengeneza fursa baina ya
nchi hizo mbili kuboresha huduma za matibabu ya moyo.
“Kama nchi tumeweza kufungua milango zaidi kusaidia nchi
nyingi za Afrika na sasa tumeenda mbali zaidi hadi Burkina Faso, yote hii
tunataka kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa kitivo cha utalii wa matibabu kwa
kutoa huduma bora zenye viwango vya kimataifa”, alisema Dkt. Asha
Dkt. Asha alisema Tanzania bado inaendelea kufungua milango
ya kushirikiana na nchi nyingine katika masuala ya kidiplomasia pamoja na afya
kwani wanatarajia kuona nchi nyingi zinafika Tanzania kwaajili ya kujifunza.
Comments
Post a Comment