Upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito na watoto mkoani Arusha



Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akigawa vipeperusha vya lishe na shinikizo la juu la damu kwa wananchi  wa mkoa wa Mbeya waliofika  kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa katika kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika hivi karibuni  katika viwanja vya City Park Garden. Jumla ya watu 751 walipata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi hiyo.

*******************************************************************************************************************************************************************************************************

Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 08/03/2025 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha  tutatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito na watoto.

 Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote ambapo Wataalamu Wanawake wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) watatoa huduma hii  tarehe 01 - 08/03/2025 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika viwanja vya TBA Kaloleni karibu na Mnara wa Mwenge  mkabala na Makumbusho ya Taifa Arusha.

 Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu ya lishe bora kwa wananchi itakayowapa uelewa wa  kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanayoweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo na wale watakaokutwa na matatizo yatakayohitaji matibabu ya kibingwa watapewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Tunawaomba wanawake, wajawazito, wazazi na walezi wenye watoto wajitokeze kwa wingi kupima afya zao kujua kama wana matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa watakaogundulika kuwa wagonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754849850  na 0752211081.

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa