JKCI yatumia akili mnemba na teknolojia za kidijitali katika matibabu ya moyo
Daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago akizungumza na mkazi wa Singida aliyefika katika banda la taasisi hiyo kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida . ****************************************************************************************************************************************************************************************************************** Na Jeremia Ombelo - Singida Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elias ...