JKCI yatoa elimu ya lishe kwa kutumia pyramid ya vyakula halisi
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akiwafundisha watoto waliotembelea banda la Taasisi hiyo makundi ya vyakula na aina ya vyakula hivyo wakati wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima mzunguko wa tumbo mwananchi alifika katika banda la Taasisi hiyo kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Afisa Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group France Kapele akiwafundisha wanafunzi kutoka shule ya Maximilian namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa dharura walipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimatai...