JKCI na Appolo Hospital kushirikiana matibabu ya moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka
Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India walipotembelea Taasisi hiyo tawi la
Oysterbay jana jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India Mrithyunjaya Kalmath akijadiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipotembelea Taasisi hiyo tawi la Oysterbay jana jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka
Hospitali ya Appolo iliyopo nchini India Ashwani Singh wakati wataalamu kutoka Hospitali
ya Appolo walipotembelea taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam
Na: JKCI
******************************************************************************************************
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya
Apollo nchini India watembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la
Oysterbay kuangalia uwekezaji uliowekezwa pamoja na maendeleo ya Taasisi hiyo.
Akizungumza na Madaktari hao jana jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
alisema mbali na kuangalia uwekezaji wa taasisi hiyo pia wamekubaliana
kushirikiana katika masuala ya upasuaji wa moyo na kubadilishana ujuzi.
Dkt. Kisenge alisema ushirikiano huo utawasaidia wataalamu wa
JKCI kupata ujuzi na kuweza kufanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa kutumia njia ya
tundu dogo kuwasaidia wagonjwa kupunguza muda wa kukaa hospitalini.
“Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Apollo iliyopo nchini
India wamekuja kujionea maendeleo makubwa yaliyofanya na Taasisi yetu katika
tawi letu la Oystebay na kuahidi kushirikiana nasi katika matibabu ya upasuaji
wa moyo kwa wagonjwa wetu” alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema sambamba na kubadilisha ujuzi JKCI na
Hospitali ya Appolo watakuwa wanabadilishana wataalamu kwa kuwapeleka Appolo na
wa Appolo kwenda JKCI kujifunza mambo mbalimbali katika kutoa huduma ya upasuaji
wa moyo.
“Kwa kufanya hivyo kutawasaidia wataalamu wetu kukutana na
wenzao kubadilishana ujuzi ili wote kwa pamoja tuweze kuokoa maisha ya wagonjwa
wetu wa moyo”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka
Hospitali ya Appolo iliyopo nchini India Mrithyunjaya Kalmath alisema amefurahi
kuona wataalamu wa Hospitali ya Appolo wanaenda kushirikiana na Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete kwani wamekuwa wakiisikia Taasisi hiyo kutokana na huduma bobezi
za matibabu ya moyo inazozifanya.
“Ushirikiano wetu utaende kurahisisha huduma za upasuaji
mkubwa wa moyo kwani tutatoa huduma hizo kwa kutumia njia ya tundu dogo na
kuwapunguzia wagonjwa maumivu na muda wa kukaa hospitali”, alisema Dkt. Kalmath
Dkt. Kalmath alisema wanaahidi kufanya kazi ya kuokoa maisha
ya wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na Taasisi hiyo na kuleta maendeleo katika
utoaji wa huduma bingwa bobezi za matibabu ya moyo.
Comments
Post a Comment