JKCI yaandaa mpango mkakati utalii tiba
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yaandaa mpango mkakati
wa utalii tiba wa kuhakikisha tiba utalii Tanzania inashika hatamu kwa kutumia
teknolojia katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi.
Mpango mkakati huo ulioandaliwa kwa siku tatu na wajumbe wa
kamati ya utalii tiba wa Taasisi hiyo umelenga kuitikia wito wa Mhe. Rais Dkt.
Samia Sululhu Hassan kuhakikisha tiba utalii Tanzania inakuwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mwenyekiti wa kamati
ya utalii tiba Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Harun Nyagori
alisema wajumbe hao wametumia siku tatu kukaa pamoja na kuandaa mpango ambao
utatoa muongozi katika kuwahudumia wagonjwa wanaotoka nchi mbalimbali kutibiwa
JKCI.
“Mpango mkakati huu tunaouandaa upo katika hatua ya kwanza,
ukishapitishwa utatoa muongozo wa namna ya kupata soko la wagonjwa kutoka
pembezoni na karibu na mipaka inayizunguka Tanzania lakini pia kutoka maeneo
mengine duniani kutibiwa katika Taasisi yetu”, alisema Prof. Nyagori
Prof. Nyagori aliushukuru uongozi wa Taasisi hiyo kuiamini na
kuiwezesha kamati ya utalii tiba kutengeneza mpango mkakati wa utalii tiba wa
kwanza utakaosimamia shughuli zote za utalii tiba katika Taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa kuandaa mpango mkakati wa
utalii tiba wa Taasisi hiyo Sylvester Nandi alisema JKCI imewekeza katika
miundombinu na wataalamu hivyo kama watafuata muongozo uliopo katika mpango
mkakati huo utalii tiba nchini utakuwa.
Nandi alisema baada ya kukaa na wajumbe wa kamati ya utalii
tiba wa JKCI ameweza kuona na kuifahamu zaidi Taasisi hiyo ambayo inatoa huduma
zinazokidhi viwango vya kimataifa.
“Kwa kipindi cha siku tatu nimekaa na wataalamu kutoka JKCI
kuandaa mpango mkakati wa utalii tiba ambapo kwa pamoja tumepitishana katika
maeneo mbalimbali na kuweka mikakati ambayo ikifuatwa itakuza utalii tiba
nchini”, alisema Nandi



Comments
Post a Comment