Dkt. Kisenge: Jitokezeni kupima moyo maonesho ya SABASABA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi mwandishi wa TBC aliyetembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya kilwa.
Mteknolojia wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Jordan Megabe akimchukuwa kipimo cha damu mwananchi aliyetembelea banda
la Taasisi hiyo kwaajili ya kumfanyia vipimo vya kuchunguza figo, ini na
kiwango cha mafuta mwilini wakati wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere vilivyopo
barabara ya kilwa.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Serikalini wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akimpatia zawadi mwananchi
aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 49 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu
Nyerere vilivyopo barabara ya kilwa.
Picha na: JKCI
*********************************************************************************************
Wakazi wa Dar es saalam na mikoa ya
karibu wametakiwa kutembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya
kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar
es Salaam (SABASABA) kwaajili ya kupima, kupata elimu, ushauri na kupata
matibabu ya moyo .
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es
saalam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu huduma wanazozitoa kwenye taasisi hiyo na
maonesho hayo kwa kuwahasa wakazi wa Dar es saalamu na mikoa ya karibu waweze
kutembelea banda la JKCI ili wapatiwe elimu na matibabu ya moyo na huduma
wanazozitoa ikiwemo ya shuka maalumu kwa wagonjwa lijulikananalo kama Dozee.
Dkt. Kisenge ambaye pia ni Daktari bingwa
wa magonjwa moyo amesema iwapo mtu atapima afya ya moyo wake mapema
itamsaidia kujua kama ana matatizo au
hana, na iwapo anamatatizo itamsaidia kujijua mapema.
“Katika maonesho haya tunatoa tiba ya
uchunguzi wa mataibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo, kwa wale watakaokutwa na shida ya moyo kwa watoto na watu wazima
tutawapa rufaa kutibiwa katika Taasisi yetu, magonjwa ya moyo ni mmoja ya
magonjwa yasioambukiza ikiwa watu watafuata mtindo bora wa maisha ikiwemo ulaji
wa mboga za majani na matunda kwa wingi”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge pia aliitaja huduma nyingine
inayopatikana katika banda hilo ni ile ya teknologia ya kisasa ya kufuatilia
hali ya mgonjwa aliyopo nyumbani kwa kutumia teknolojia ya Dozee ambayo
inamsaidia Daktari kwa haraka kupata hali halisi ya wagonjwa mara baada ya kufanyiwa
upasuaji. Teknologia hiyo ya dozee ambayo ni shuka maalumu inayotandika chini
ya kitanda cha mgonjwa inamuwezesha Daktari kujua hali ya upumuaji, presha ya
mgonjwa na mapigo ya moyo ya mgonjwa aliyopo nyumbani.
Mwananchi aliyepatiwa huduma ya
uchunguzi na matibabu ya moyo katika banda hilo Fortunatus Michael alishukuru
kwa huduma ya matibabu aliyopata na kusema kuwa imemsaidia kujua afya ya moyo
wake.
“Ninawahamasisha watu waje kutembelea
na kupatiwa huduma ya matibabu ya moyo katika banda la JKCI wakati huu wa maonesho
ya SABASABA kwani huduma zinatolewa kwa gharama nafuu kuliko ukienda hospitali”
alisema Fortunatus
“Nawaomba wananchi wenzangu mje
mtembelee banda la Taasisi ya moyo mfanyiwe uchunguzi na matibabu ya moyo kwani
gharama ni nafuu ukilinganisha na hospitalini” alisema Fortunatus
Kila mwaka Taasisi ya moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) imekuwa ikishiriki kwenye maonesho ya sabasaba kwa kutoa huduma
za kibigwa za upimaji na matibabu ya moyo ili kuwarahisishia wananchi kupata
huduma hizo.
Comments
Post a Comment