Wafanyakazi wa JKCI wafundishwa namna ya kudhibiti wa msongo wa mawazo

Mtaalamu wa Saikolojia na Mahusiano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Chris Mauki akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo pamoja na kuweka mipaka ya kazi na mambo binafsi. Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika hivi karibuni  katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa mafunzo ya udhibiti wa msongo wa mawazo yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza mafunzo ya udhibiti wa msongo wa mawazo yaliyokuwa yanatolewa na Mtaalamu wa Saikolojia na Mahusiano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Chris Mauki. Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika hivi karibuni  katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa