Mwenyekiti wa Bodi ya Heart
Team Africa Foundation (HTAF) Mhe. Mussa Zungu akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha bodi ya
wakurugenzi wa Heart team Africa Foundation (HTAF) kilichofanyika Protea Hotel iliyopo Jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Mhe. Mussa Zungu akiwa kwenye picha ya Pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Heart Team Africa Foundation (HTAF) baada ya kikao cha kwanza cha bodi ya wakurugenzi katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Heart Team Africa Foundation (HTAF) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa Majani wakati akitoa ripoti kuhusu taasisi hiyo katita hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Mhe. Mussa Zungu na moja ya muasisi wa Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Peter Kisenge wakisikiliza maoni ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi katika kikao cha kwanza cha Heart team Africa Foundation (HTAF) kilichofanyika Protea Hotel iliyopo Jijini Dar es Salaam.
*************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Taasisi
isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) imetoa wito kwa
wananchi kuunga mkono taasisi hiyo kwakuchangia matibabu ya magonjwa ya moyo
kwa watoto na kuokoa maisha yao kwa wale wasioweza kumudu gharama za matibabu.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Mhe.
Mussa Zungu huku wakiwa na jukumu la kusimamia na kuratibu mikatati ya
kuwasaidia wanachi wenye matatizo ya moyo hususani watoto.
Akizungumza
wakati wa mkutano wa taasisi hiyo hii leo Mwenyekiti wa Bodi ya Heart Team
Africa Foundation (HTAF) Mhe. Mussa Zungu alisema kuwa zaidi ya watoto 13,800
huzaliwa kila mwaka wakiwa na matatizo ya moyo na wengi wao hawana uwezo wa
kugharamia matibabu hayo.
“Tunatakribani
watoto elfu 13,800 kwa mwaka wanaozaliwa na shida ya moyo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia
anachangia asilimia 70 ya gharama za matibabu, gharama za kumtibu mtoto mmoja
ni kati ya Shilingi milioni nane hadi tisa.” Alisema Mhe. Zungu.
Aidha,
alieleza kuwa taasisi hiyo inawasaidia watoto wenye magonjwa ya moyo kutokana
na misaada ya wafadhili waliochangia zaidi ya Shilingi bilioni 3 na milioni 200
ili kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo.
“Bodi
hii inaishi kutokana na michango ya wafadhili wa ndani na nje, tunawashukuru
waliotuchangia bilioni 3 na milioni 200 kupitia harambee maalum ya kuchangia
watoto wenye matatizo ya moyo,” aliongeza Zungu.
Mhe.
Zungu alitoa wito kwa Watanzania kuungana na Serikali katika kusaidia juhudi za
kuokoa maisha ya watoto kupitia mchango wao wa hiari.
“Hakuna
sababu ya mtoto wa Kitanzania kufa kwa sababu ya ugonjwa wa moyo watanzania
kushirikiana na Dkt. Samia na serikali yake tuunge mkono taasisi hii ili kuokoa
maisha ya watoto wetu,” alisisitiza Mhe. Zungu.
Nae
Mtendaji Mkuu wa Heart Team Africa Foundation Dkt. Naizihijwa Majani alieleza
kuwa katika mkutano huo wamejadili mkakati wa miaka minne wenye lengo la
kusaidia wagonjwa wa moyo na kuisaidia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
pamoja na taasisi nyingine katika tafiti kuhusu magonjwa ya moyo.
“Leo
tumepitia mpango mkakati wa miaka minne na wa mwaka mmoja jukumu letu kubwa ni
kukusanya fedha kusaidia wasiokuwa na uwezo kwenye matibabu ya moyo na kufanya
tafiti ili kusaidia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na taasisi nyingine,”
alisema Dkt.Naiz.
“Tutaendelea
kutoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa jamii na pia kuwajengea uwezo watumishi wa
afya kutoka hospitali ya JKCI ili kuwasaidia watoto na watu wazima wanaopata
matibabu ya moyo,” aliongeza Dkt.Naiz.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),
Dkt. Peter Kisenge alieleza kuwa uanzishwaji wa HTAF ni sehemu ya mkakati wa
kusaidia watoto wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu ya moyo.
“Katika
watoto 100 wanaozaliwa nchini kati ya mmoja au wawili huwa na magonjwa ya moyo
na wengi hawana uwezo wa kulipia gharama za matibabu ndiyo maana bodi ya
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliridhia kuanzishwa kwa Taasisi isiyo ya
kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) ili kusaidia watoto hao,”
alisema Dkt. Kisenge.
“Moja
ya malengo yetu makubwa ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu afya ya moyo,
kuhamasisha watu kuchangia ili kusaidia wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama
za matibabu ya moyo,” aliongeza Dkt.Kisenge.
HTAF
imeahidi kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na wadau wote wa afya ili kuhakikisha
watoto wote wenye matatizo ya moyo wanapata matibabu, bila kujali uwezo wao wa
kifedha.
Comments
Post a Comment