Global Fund watembelea JKCI kuangalia mtambo wa Oksijeni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana
na Ukimwi, Kifua kikuu na Ukoma (Global Fund) walipotembelea Taasisi hiyo jana
kwaajili ya kuangalia mtambo wa Oksijeni uliosimikwa katika Taasisi hiyo
iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa vifaa tiba kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) Eng. Abela Rweguza akiwaelezea viongozi kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua kikuu na Ukoma (Global Fund) namna ambavyo JKCI imefaidika na mtambo wa Oksijeni uliosimikwa JKCI wakati wa ziara yao jana kuangalia namna unavyofanya kazi.
Msimamizi wa chumba cha uangalizi maalumu cha watoto wenye
magonjwa ya moyo (ICU) Mohamed Wamara akiwaelezea namna oksijeni inavyowafikia
watoto waliolazwa ICU viongozi kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua
kikuu na Ukoma (Global Fund) walipotembelea Taasisi hiyo jana kuangalia namna
mtambo wa Oksijeni uliosimikwa JKCI unavyofanya kazi.
Mhandisi wa vifaa tiba kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Eng. Veronica Mugendi akiwaonesha baadhi ya mitungi iliyojaa oksijeni viongozi kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma (Global Fund) walipotembelea Taasisi hiyo jana kuangalia namna mtambo wa Oksijeni uliosimikwa JKCI unavyofanya kazi.
Picha na: JKCI
*********************************************************************************************************
Comments
Post a Comment