
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ditram Mgimba akimpima uwiano wa urefu kwa uzito (BMI) mkazi wa Dar es Salaam aliyefika katika viwanja vya Police Office Mess Oysterbay wakati wa bonanza la NBC kuelekea mbio za NBC zitakazofanyika Julai 26 mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI
Daktari
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Moris Budotela akimuelezea umuhimu
wa kupima afya mkazi wa Dar es Salaam aliyefika katika viwanja vya Police
Office Mess Oysterbay wakati wa bonanza la NBC kuelekea mbio za NBC
zitakazofanyika Julai 26 mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto
wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI.
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ditram Theodory Mgimba akimpima
shinikizo la damu mkazi wa Dar es Salaam aliyefika katika viwanja vya Police
Office Mess Oysterbay wakati wa bonanza la NBC kuelekea mbio za NBC zitakazofanyika
Julai 26 mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya
moyo wanaotibiwa na JKCI.
Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina
Komba akimfanyia usajiri mkazi wa Dar es Salaam aliyefika katika viwanja
vya Police Office Mess Oysterbay wakati wa bonanza la NBC kuelekea mbio za NBC
zitakazofanyika Julai 26 mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto
wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sahiya Yahya akimpatia
ushauri mara baada ya kufanya uchunguzi wa afya mkazi wa Dar es Salaam aliyefika
katika viwanja vya Police Office Mess Oysterbay wakati wa bonanza la NBC
kuelekea mbio za NBC zitakazofanyika Julai 26 mwaka huu kwaajili ya kuchangia
matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI.
Na JKCI
*******************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Watu zaidi ya 50 wamefanyiwa uchunguzi wa afya kuelekea mbio za NBC zitakazofanyika Julai 26 mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Uchunguzi huo umefanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Bonanza la NBC lililofanyika leo katika viwanja vya Police Office Mess vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Watu hao wamefanyiwa uchunguzi wa afya kwa kupimwa shinikizo la damu (BP), kiwango cha sukari kwenye damu, uzito, urefu pamoja na uwiano wa uzito kwa urefu (BMI) kama sehemu ya kutathmini hali zao za kiafya na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.
Akizungumza wakati wa Bonanza hilo Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Moris Budotela alisema kati ya watu waliofika kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya, watu wanne walibainika kuwa na changamoto za kiafya zilizohitaji ufuatiliaji zaidi hivyo kupewa rufaa ya kufika katika Taasisi hiyo kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Aidha Dkt. Moris alisema tatizo kubwa ambalo limekuwa likibainika mara kwa mara wataalamu wanapoweka kambi za uchunguzi wa afya ni tatizo shinikizo la damu hivyo kuiomba jamii kuendelea kufanya uchunguzi wa afya wa mapema na kuchukua hatua.
Kwa upande wake Juma Kisuma mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam aliyeshiriki bonanza hilo alisema kuchunguza kwake afya kumemsaidia kujitambua na kuona umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.
“Tunaishukuru JKCI kwa kufanya zoezi la kutupima afya katika bonanza hili kwani huduma hizi ni muhimu kwetu sote ,” alisema Kisuma
Comments
Post a Comment