Mhe. Fatma Nyangasa awahamasisha wananchi kupima afya kupitia Kampeni ya Jua Namba Zako
Daktari bingwa wa
upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thabit Ramadhani
akumueleza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa namna moyo
unavyofanya kazi alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho
ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika
viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini
Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idd Kimario akimpima Shinikizo la damu Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya
Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa akitazama mfano wa saani ya makundi ya
chakula alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo
katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya
Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa akipokea zawadi kutoka kwa daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce
alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Na JKCI
*******************************************************************************************
Wananchi
wametakiwa kutumia fursa ya Maonesh ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam
(SABASABA) kutembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili kupima
afya zao na kutambua mapema vihatarishi vya magonjwa ya moyo na magonjwa
mengine yasiyoambukiza kupitia kampeni ya Jua Namba Zako.
Wito huo
umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa alipotembelea
banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
lililopo katika maonesho hayo na kuweza kujua namba zake.
Mhe. Fatma
alisema JKCI imewaletea wananchi huduma muhimu zinazowawezesha kufanya
uchunguzi wa afya, lakini pia kupata elimu ya kujikinga na magonjwa ya moyo.
“Kuna vitu vingi vya faida katika
banda hili kuna huduma zote za msingi zinazohusiana na masuala ya moyo, lakini
pia huduma nyingine muhimu za afya zinazopatikana kwa urahisi”, alisema Mhe.
Fatma
Aidha Mhe.
Fatma alisema kampeni ya Jua Namba Zako ni ya muhimu kwa kuwa inawahamasisha
wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara badala ya kusubiri hadi
wanapoumwa.
“Mimi tayari nimezijua
namba zangu, fika kwenye banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete upime urefu,
uzito, shinikizo la damu na vipimo vingine muhimu ili ujue hali yako ya afya”,
alisema Mhe. Fatma
Vile vile Mhe.
Fatma aliipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kuifanya Taasisi
hiyo kuwa miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma za kisasa za matibabu ya moyo.
Mbali na
kampeni ya Jua
Namba Zako, Mhe. Fatma aliwahamasisha wananchi kuendelea kushiriki
katika kampeni ya Kutoa ni Moyo inayolenga kuchangisha fedha za kuwasaidia
watoto wenye matatizo ya moyo kupata matibabu katika Taasisi hiyo.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Comments
Post a Comment