Posts

UZINDUZI WA KAMPENI YA TEMBEA NA JKCI LINDA MOYO WAKO

Image
Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mahali ambapo uzinduzi wa kampeni ya Tembea na JKCI linda moyo wako utafanyika ****************************************************************************************************************************** TAARIFA KWA UMMA   UZINDUZI WA KAMPENI YA TEMBEA NA JKCI LINDA MOYO WAKO Katika utekelezaji wa mpango wa taifa wa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  itazindua  matembezi ya kilomita tano (5KM) kwa ajili ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi duniani. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 02/12/2022 majira ya saa 10 jioni katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Upanga jijini Dar es Salaam. Baada ya uzinduzi kutakuwa na  matembezi ya umbali wa kilomita tano (5KM) yatakayoanzia JKCI kupita mitaa ya Kalenga, Barabara za Umoja wa Mataifa, Bibi Titi, Magore, Malick na kuis...

Kuwait, JKCI kuimarisha matibabu ya moyo kwa watoto

Image

Kwa mara ya kwanza madaktari wazawa wa JKCI wafanya upasuaji wa kubadilisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta)

Image
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akimuelekeza mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kubadilisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao unatoka kwenye moyo mpaka sehemu inayotoa matawi ya mishipa inayopeleka damu kwenye kichwa na ubongo (ascending aorta and arch) Mohamed Dinya kufanya zoezi la kupuliza mashine ijulikanayo kwa jina la Spirometer kwa ajili ya kupanua mapafu baada ya kufanyiwa upasuaji huo ************************************************************************************************** Madaktari wazawa mabingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kubadilisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao unatoka kwenye moyo mpaka sehemu inayotoa matawi ya mishipa inayopeleka damu kwenye kichwa na ubongo (ascending aorta and arch). Upasuaji huo unaojulikana kwa jina la kitaalamu la Bental Procedure and hemi-arch aortic...

Kuwait, JKCI kuimarisha matibabu ya moyo kwa watoto

Image
  Daktari bingwa wa usingizi kutoka Shirika linalotoa msaada wa matibabu ya moyo kwa watoto la Children’s Heart Charity Association lililopo nchini Kuwait Hesham Menshawy akielezea namna ambavyo shirika hilo litashirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto walipotembelea JKCI leo jijini Dar es Salaam. Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na mwenzao kutoka Shirika linalotoa msaada wa matibabu ya moyo kwa watoto la Children’s Heart Charity Association lililopo nchini Kuwait Dkt. Faisal Al-Saiedi kuangalia picha ya tundu lililopo kwenye moyo kwa kutumia mashine ya Trans esophageal ECHO kwa mtoto ambaye anarudiwa upasuaji wa moyo wa kuziba tundu na valvu inayovuja walipotembelea JKCI kwa kuangalia namna ya   kushirikiana na Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.  Daktari bingwa wa Upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiwaelezea aina...

Upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo katika mikoa ya Mtwara na Lindi

Image
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulwa Richard akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya siku tano iliyofanyika mwezi wa Oktoba katika Hospitali hiyo. *********************************************************************************************************************************************************************************   TAARIFA KWA UMMA   UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara pamoja na  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine   watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima. Mkoani Mtwara upimaji utafanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Novemba, 2022 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika viwanj...

JKCI yaanzisha kliniki ya maumivu ya kifua

Image
  Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo Upanga Jijini Dar es Salaam ambapo huduma zote za matibabu ya moyo zinatolewa. *************************************************************************************************************************************************************************************************************************************** Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha kliniki ya matibabu ya maumivu ya kifua kwa wagonjwa wenye   maumivu ya vichomi kifuani na kifua kubana ili waweze kufanyiwa uchunguzi wa haraka kwani maumivu hayo huambatana na magonjwa mbalimbali ya moyo ikiwemo shambulio la moyo. Akizungumzia leo kuhusu kliniki hiyo inayofanyika JKCI iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo wa Taasisi hiyo Dkt. Tatizo Waane alisema kuwepo kwa huduma hiyo kutawafanya wagonjwa kupata huduma ya matibabu mapema. Dkt. Waane ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema maumivu ya kifua yamekuwepo ka...

JKCI yaja na kampeni ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kujikinga na magonjwa ya moyo

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea leo jijini Dar es Salaam maT- shirt mawili kati ya 100 kutoka kwa Meneja mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya K4S Security Kemmy David zitakazotumika wakati wa matembezi ya Km.5 kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo. Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Ulinzi ya K4S Security Joseph Goliama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge leo jijini Dar es Salaam baadhi ya maT-shirt kati ya 100 yaliyotolewa na Kampuni hiyo zitakazotumika wakati wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Kampuni ya Ulinzi ya K4S Security walipotembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kumkabidhi T-shirt 100 ...