JKCI yapeleka huduma za moyo ndani ya Treni ya SGR kwa mara ya kwanza
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Yvone
Mushi akimsomea majibu ya kipimo cha shinikizo la damu (BP) abiria aliyesafiri
na treni ya mwendokasi (SGR) wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu
ya magonjwa ya moyo inayofanyika katika treni hiyo katika kuadhimisha siku ya
moyo duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 mwezi Septemba.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes
Lugendo akimuuliza maswali ya ufahamu abiria aliyesafiri na treni ya mwendokasi
(SGR) wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo
inayofanyika katika treni hiyo katika kuadhimisha siku ya moyo duniani ambayo
uadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 mwezi Septemba.
Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Yatimuni Mushi akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO)
abiria aliyesafiri na treni ya mwendokasi (SGR) wakati wa kambi maalumu ya
uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo inayofanyika katika treni hiyo katika
kuadhimisha siku ya moyo duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 29
mwezi Septemba.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joel Joel
akizungumza na abiria aliyesafiri na treni ya mwendokasi (SGR) wakati wa kambi maalumu
ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo inayofanyika katika treni hiyo
katika kuadhimisha siku ya moyo duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe
29 mwezi Septemba.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli
Msigwa akimsikiliza abiria aliyesafiri na treni ya mwendokasi (SGR) mara baada
ya kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu
ya magonjwa ya moyo inayofanyika katika treni hiyo katika kuadhimisha siku ya
moyo duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 mwezi Septemba.
Na JKCI
********************************************************************************************************************
Kwa mara ya kwanza huduma za uchunguzi na matibabu ya
magonjwa ya moyo zimeanza kutolewa ndani ya treni ambapo wasafiri wanaotumia
treni ya mwendokasi (SGR) ufanyiwa uchunguzi wa magonjwa hayo wakati wa safari.
Huduma hiyo inatolewa kupitia kambi maalumu ya siku saba
inayofanywa na Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha
siku ya moyo duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 mwezi Septemba.
Akizungumza wakati wa kambi hiyo daktari wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Samweli Msigwa alisema huduma hizo zinatolewa kwa abiria
wanaosafiri na treni ya SGR ikiwa ni sehemu ya kuisogozea jamii huduma za
kibingwa karibu.
Dkt. Samweli alisema jamii imekuwa ikitumia muda mwingi
kufanya shughuli mbalimbali na kukosa muda wa kupima afya zao lakini kupitia
kambi hiyo abiria wa SGR wamejitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa afya.
“Tumeanza kuona mafanikio ya kambi hii mapema leo ikiwa ni
siku ya kwanza, abiria wanaosafiri na Treni ya SGR wamefurahishwa na uwepo
wetu, wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao na hii inaonesha kuwa uhitaji ni
mkubwa”, alisema Dkt. Samweli
Kwa upande wao abiria wanaosafiri na Treni ya SGR
wameishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Reli Tanzania
(TRC) kuona umuhimu wa kuwafikishia huduma hizo wakati wa safari kwani ni kweli
kutokana na shughuli mbalimbali za maisha wamekuwa wakishindwa kufika hospitali
kwaajili ya kufanya uchunguzi wa afya.
Mwifadhi Mrisho akiwa katika treni hiyo kuelekea Mkoani Morogoro
alisema huduma za uchunguzi wa afya ni za nadra hivyo zinapojitokeza ni fursa
kwa jamii kujua afya zao, kupata elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa
mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo.
“Natamani zoezi hili liwe endelevu kila tukipanda treni
tukutane na huduma za uchunguzi wa afya kwani mnatusaidia sana na kuokoa maisha
yetu”, alisema Mwifadhi
Mwifadhi alisema huduma hizo angeenda kuzipata hospitalini
angetumia muda mwingi na gharama kubwa lakini kupitia kambi hiyo amefanyiwa
vipimo vya moyo bila gharama.
Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa
Luzineth Kingamkoni ameuomba uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuweka
huduma za uchunguzi wa matibabu ya moyo katika treni zake zote ili kila
mwananchi afikiwe na huduma hizo.
“Nawaomba wasafiri wenzangu wawe tayari kupima afya zao kwani
wataalamu wanatoa huduma bora, rahisi, na inatuwezesha kukagua afya zetu na
kuwa salama”, alisema Askofu Luzineth
Comments
Post a Comment