Huduma za matibabu ya moyo zawafuata wananchi wa Geita

 

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Moses Manumbu akizungumza na mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita

Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Victoria Kazibila akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography- ECG) mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abdull Mohamed akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyefika katika banda la KCI wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya Tekinologia ya madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita.

Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akimpima mzunguko wa kiuno mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita


 Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita wakisubiri kupata huduma za vipimo walipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya tisa ya kitaifa ya Tekinologia ya madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita.

Picha na JKCI.

**************************************************************************                                         ***************************

Wananchi wa Geita wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yakiwemo ya moyo ili kujikinga na vifo vya gafla vinavyoweza kusababishwa na kutokufanya uchunguzi wa mapema.

Rai hiyo imetolewa leo na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Kariakoo Moses Manumbu wakati wa maonesho ya tisa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassani mkoani Geita.

Dkt. Manumbu alisema uchunguzi wa afya mapema husaidia kubainia na kuthibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo shinikizo la juu la damu ambalo ni miongoni mwa magonjwa yanayoweza kusababisha madhara makubwa na kuua kimyakimya.

 “Hii ni fursa kwa wananchi wa Geita na mikoa ya jirani kujitokeza katika banda la JKCI kufanya uchunguzi wa afya bila malipo na kupata elimu ya namna ya kujilinda na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanaongoza kwa vifo vingi duniani”, alisema Dkt. Manumbu

Dkt. Manumbu aliongeza kuwa wananchi watakaobainika kuwa na matatizo ya moyo yanayohitaji matibabu ya kibingwa au upasuaji watapatiwa rufaa ya kwenda JKCI kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na wengine kupatiwa matibabu.

Baaadhi ya wananchi waliofika katika banda la JKCI kwaajiili ya kufanya uchunguzi wa afya wameipongeza JKCI kwa kuendelea kuwajali wananchi wa Geita kwa kufikisha huduma hizo katika kila maonesho ya madini na kuwahudumia wananchi hususani wale ambao hawana uwezo wa kugharamia vipimo.

“Tumepokelewa na kupata huduma nzuri za uchunguzi wa magonjwa ya moyo ikiwemo kisukari na shinikizo la damu, naomba wale ambao bado wanasita kufika katika viwanja hivi wafanye maamuzi na wajitokeze kujua hali zao za afya”, alisema Tecla John mkazi wa Geita.

Naye Michael Buganda mkazi wa Geita vijini alisema amefurahishwa na huduma alizozipata pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.

“Nimefurahi kukutana na daktari wa moyo ambaye ameongea na mimi vizuri na kunipa ushauri ambao utanisaidia kwa wale wote ambao tumefanyiwa uchunguzi wa awali na kuandikiwa dawa tumehamasishwa tuhakikishe tunatafuta dawa hizo na kuzitumia”, alisema Michael

JKCI imekuwa ikishiriki katika maonesho ya madini ambayo yamekuwa yakifanyika mkoani Geita kila mwaka lengo likiwa kusogeza huduma bingwa bobezi za uchunguzi wa magonjwa ya moyo karibu na wananchi.





Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma