JKCI mshindi wa kwanza Taasisi inayoboresha huduma na kutoa huduma bora kwa jamii

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akimpatia tuzo ya mshindi wa kwanza Taasisi zinazoboresha huduma na kutoa huduma bora kwa jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi, mashirika ya umma na wakala wa serikali (CEO Forum 2026) kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Florence Samizi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge mara baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa kwanza Taasisi zinazoboresha huduma na kutoa huduma bora kwa jamii iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi, mashirika ya umma na wakala wa serikali (CEO Forum 2026) kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Na: JKCI

**********************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi zinazoboresha huduma na kutoa huduma bora kwa jamii. Ushindi huo umetangazwa leo wakati wa kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi, mashirika ya umma na wakala wa serikali (CEO Forum 2026) kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Katika kutambua mchango wa Taasisi hiyo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius John Ndejembi alitoa tuzo kwa Taasisi hiyo iliyothamini matumizi ya huduma za kidijitali, kiwango cha kuridhika kwa wateja pamoja na ukuaji wa wateja katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Akizungumza Baada ya kupata tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema ushindi huo ni matokeo ya juhudi ya taasisi katika kuendelea kuboresha huduma, kutumia teknolojia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazokidhi mahitaji yao.

“Tuzo hii ni ushahidi wa kazi kubwa inayofanywa na watumishi wa JKCI kwa moyo, nidhamu na kujitolea, mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za kila mmoja wetu na nguvu ya timu yetu”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge aliongeza kuwa tuzo hiyo inapaswa kuwa chachu kwa JKCI kuendelea kuweka viwango vya juu katika utoaji wa huduma kuwahudumia wadau kwa uadilifu na kuhakikisha taasisi hiyo inaendelea kuwa mfano wa ubora nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma