Wataalamu wa afya kutoka nchini Tanzania, Kenya, Eswatini Botswana na Malawi washiriki mafunzo ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto

 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naizihijwa Majani akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto (Paediatric Echocardiography) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Engerasia Kifai akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto (Paediatric Echocardiography) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wataalamu wanaoshiriki mafunzo ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto (Paediatric Echocardiography) yanayotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naizihijwa Majani, Mkurugenzi wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI Dkt. Engerasia Kifai, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI Dkt. Sulende Khuboja na baadhi ya wataalamu wanaoshiriki mafunzo ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto (Paediatric Echocardiography) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha Na

*****************************************************************************************************************************************

Waaatalamu 21 wa afya kutoka nchini Tanzania, Kenya, Eswatini Botswana na Malawi kunufaika na mafunzo ya siku 10 ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto (Paediatric Echocardiography).

Mafunzo hayo yanayotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni hatua ya kuongeza wataalamu wenye uwezo wa kugundua magonjwa ya moyo kwa watoto mapema na kuwajengea uwezo wataalamu hao kufanya uchunguzi wa awali wa magonjwa ya moyo kwa watoto katika vituo vyao vya kutolea huduma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naizihijwa Majani alisema mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za kusogeza huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto karibu na wananchi hususani katika hospitali za mikoa na wilaya.

“Mafunzo haya yatawezesha wataalamu kupata ujuzi, na kuweza kugundua magonjwa ya moyo kwa watoto mapema hivyo kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa wakati”, alisema Dkt. Naizihijwa.

Dkt. Naizihijwa ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto alisema washiriki watakaporejea katika maeneo yao ya kazi watatumia ujuzi walioupata kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto lakini pia kuwafundisha wataalamu wenzao hivyo kuongeza wigo wa huduma hiyo nchini.

Dkt. Naizihijwa aliongeza kuwa JKCI imepanga kuendelea kutoa mafunzo hayo kila baada ya miezi mitatu ili kuwafikia wataalamu wengi zaidi na kuongeza uwezo wa kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Engerasia Kifai alisema kuanzishwa kwa kozi hiyo kumelenga kukabiliana na uhitaji mkubwa wa wataalamu wenye ubobezi katika uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto.

“Tunataka kurahisisha ugunduzi wa matatizo ya moyo kwa watoto kwa haraka kwa sababu unapogundua mapema matatizo hayo ni rahisi kuanzisha matibabu sahihi na wale wanaohitaji upasuaji, upasuaji wao unaweza ukafanyika vizuri na kuwa na matokeo mazuri”, alisema Dkt. Kifai.

Naye Msaidizi wa Kliniki ya Watoto kutoka Hospitali ya Kamuzu Central ya nchini Malawi Treasure Mkaliainga alisema mafunzo hayo yatamwezesha kuongeza ujuzi wa kufanya uchunguzi sahihi wa magonjwa ya moyo kwa watoto.

“Mafunzo haya ni muhimu kwangu kwasababu yatanipa ujuzi unaohitajika kufanya uchunguzi sahihi wa magonjwa ya moyo kwa watoto jambo ambalo litatusaidia kuandaa mipango sahihi ya matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo”, alisema Treasure.

JKCI itaendelea kutoa mafunzo hayo ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto (Paediatric Echocardiography) kila baada ya miezi mitatu ili kuongeza ujuzi kwa wataalamu wa afya kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.


Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma