Wananchi Geita waipongeza JKCI kwa huduma bingwa na bobezi za moyo.


 Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Moses Manumbu akisikiliza mapigo ya moyo ya mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita.


Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akimpima urefu mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abdull Mohamed akimpima kiwango cha sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili mjini Geita. 

Picha JKCI.

************************************************************************************************

Wananchi wa Mkoa wa Geita wameishukuru na kuipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya tekinologia ya madini.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali waliofika katika banda la JKCI na kufanyiwa uchunguzi wa afya ikiwemo kupimwa kiwango cha sukari kwenye damu, shinikizo la damu, mzunguko wa kiuno, vipimo vya moyo pamoja na uwiano wa uzito kwa urefu.

Rose Egatha mkazi wa Geita mjini alisema amefika katika banda hilo baada ya kupata taarifa kuhusu uwepo wa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa sababu amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kifua ya muda mrefu.

 “Nawashukuru sana JKCI kwa kutuletea huduma hizi kwani zimenisaidia kujua tatizo langu la moyo, kabla ya hapo nilikuwa nikimeza dawa mbalimbali bila kupima hivyo nashauri wananchi wenzangu tusimeze dawa bila kupata vipimo na ushauri wa dakatari”, alisema Rose.

Aisha Ramadhani Mkazi wa kalangalala aliishukuru serikali kwa kusogeza huduma za kibingwa za matibabu ya moyo karibu na maeneo yao na kuiomba iendelea kuwajali wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa kwani nimekuwa nikisikia kuhusu JKCI kupitia vyombo vya habari hivyo maonesho haya yamekuwa yakipekee kwangu na yameniletea matumaini makubwa juu ya afya yangu”, alisema Aisha.

Naye Idrisa Ntarembo Mkazi wa Nyamalembo alisema amefarijika kupata ushauri wa lishe bora kutoka kwa dakatri bingwa wa moyo nakuahidi kuufanyia kazi.

“Ushauri niliopewa utanisaidia kulinda afya ya moyo wangu sambamba na hilo nimepewa dawa za kutibu tatizo la shinikizo la damu hivyo ningependa kuwashauri wananchi wenzangu watumie fursa hii ya maonesho kufanya uchunguzi wa afya ili wajue hali zao za kiafaya”, alisema Idrisa.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inashiriki katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa  ya tekinolojia ya madini kwa kuwafanyia wananchi uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo.


Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma