UZINDUZI WA KAMPENI YA TEMBEA NA JKCI LINDA MOYO WAKO


Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mahali ambapo uzinduzi wa kampeni ya Tembea na JKCI linda moyo wako utafanyika

******************************************************************************************************************************

TAARIFA KWA UMMA

 

UZINDUZI WA KAMPENI YA TEMBEA NA JKCI LINDA MOYO WAKO

Katika utekelezaji wa mpango wa taifa wa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itazindua  matembezi ya kilomita tano (5KM) kwa ajili ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi duniani.

Uzinduzi huo utafanyika tarehe 02/12/2022 majira ya saa 10 jioni katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Upanga jijini Dar es Salaam. Baada ya uzinduzi kutakuwa na matembezi ya umbali wa kilomita tano (5KM) yatakayoanzia JKCI kupita mitaa ya Kalenga, Barabara za Umoja wa Mataifa, Bibi Titi, Magore, Malick na kuishia JKCI.

Tunawaomba wananchi muungane nasi katika matembezi haya ili tuweze kufanya mazoezi ya pamoja ambayo yatatusaidia kujikinga na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza yakiwemo ya moyo. Magonjwa haya yanaweza kuzuilika kama jamii itafuata mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi, kutokutumia bidhaa za tumbaku, kula mlo bora pamoja na kuacha kutumia vilevi ambavyo ni hatari kwa afya ya moyo.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0715288770 Oliver Marandu, 0713465963 Abdulrahman Muya na 0782042019 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). 


“Tembea na JKCI, Linda Moyo Wako”.

 Imetolewa na:


Anna Nkinda

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari