Wanafunzi wa shule ya awali na msingi Libermann watoa msaada
Wahitimu
wa darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi ya Libermann wakimkabidhi moja
ya zawadi mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Pili Mwinyimkuu ikiwa ni sehemu ya kurudisha
shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule ya msingi leo katika wodi ya
watoto wenye magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam.
Wahitimu
wa darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi ya Libermann wakimkabidhi moja
ya zawadi mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Neema Ryoba ikiwa ni sehemu ya kurudisha
shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule ya msingi leo katika wodi ya
watoto wenye magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Idara ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salma Wibonela akiwaelekeza
wahitimu ya darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi Libermann jinsi ya
kutumia mashine ya Defibrillator inayotumika kuustua moyo pale ambapo mapigo ya
moyo yapo juu sana na utendaji wake haupo vizuri walipotembelea Taasisi hiyo
kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo ikiwa ni
sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule ya
msingi.
Mteknolojia
mionzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idrisa Juma akiwaonyesha
wahitimu wa darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi Libermann namna
ambavyo mashine ya X-ray inafanya uchunguzi wa matatizo mbalimbali
walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto wanaotibiwa
katika Taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii baada ya
kumaliza salama shule ya msingi.
Mhitimu
wa darasa la saba shule ya awali na msingi ya Libermann Raphael Victor akiuliza
maswali wakati wahitimu hao walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa
zawadi kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule
ya msingi.
Wahitimu
wa darasa la saba shule ya awali na msingi Libermann wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wazazi wao baada ya kutoa zawadi kwa watoto wanaotibiwa
katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni sehemu ya kurudisha
shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule ya msingi.
Picha
na: Khamis Mussa
******************************************************************************************
Comments
Post a Comment