Madaktari bingwa wa moyo waendelea kutoa huduma za matibabu ya moyo Mkoani Geita


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Macklina Komba akimfanyia usajili mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) wakiwafanyia vipimo vya awali wananchi waliofika katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akimwelezea namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulwa Richard akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) John Daniel akimpima Shinikizo la damu mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Geita wakiwa katika foleni ya kupatiwa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH).

Picha na JKCI


 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi

Msumbiji kushirikiana na JKCI katika tiba ya moyo