JKCI yatoa mafunzo uchunguzi moyo wa watoto
Madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Stella Mongella na John King’ori kutoka Hospitali ya Dian Beach ya nchini Kenya wakifundishwa na madaktari kutoka Germany Society for Tropical Pediatrics and International Child Health (GTP) jinsi ya kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Pediatric Echocardiography). Mafunzo hayo ya siku tano yanahudhuriwa na wataalamu wa afya 22, watano kutoka Bara la Ulaya, mmoja nchini Kenya na 16 kutoka Hospitali mbalimbali hapa nchini yanatolewa na JKCI kwa kushirikiana na GTP na Chama cha madaktari wa watoto Tanzania.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifundishwa na madaktari kutoka Germany Society for Tropical Pediatrics and International Child Health (GTP) jinsi ya kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Pediatric Echocardiography). Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika JKCI yanahudhuriwa na wataalamu wa afya 22, watano kutoka Bara la Ulaya, mmoja nchini Kenya na 16 kutoka Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Daktari bingwa wa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kiwete (JKCI) Vivian Mlawi akifundishwa na madaktari kutoka Germany Society for Tropical Pediatrics and International Child Health (GTP) jinsi ya kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Pediatric Echocardiography). Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na JKCI kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani na Chama cha madaktari wa watoto Tanzania na kuhudhuriwa na wanafunzi 22 watano kutoka Bara la Ulaya, mmoja nchini Kenya na 16 kutoka Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Picha na Khamisi Mussa
Comments
Post a Comment