Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Kaspar Mmuya atembelea banda la JKCI katika mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Kaspar Mmuya akizungumza kuhusu umuhimu wa kutoa elimu kwa umma ya magonjwa ya moyo alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza unaofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Malaika jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akiwaeleza baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Mwanza kuhusu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza unaofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Malaika jijini Mwanza. 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lawrence Madole maarufu kama Marlaw akiwasikiliza Daktari Janeth Mmari na Afisa Muuguzi Tunzo Mcharo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimwelezea kuhusu madhara ya mshipa wa damu wa moyo kuziba wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza unaofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari