Posts
Upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo mkoani Kilimanjaro
- Get link
- X
- Other Apps
Wagonjwa kutoka nje ya nchi wafurahia huduma bora za matibabu ya moyo zinazotolewa JKCI
- Get link
- X
- Other Apps

Mwananchi kutoka nchini Malawi Jane Chimuyaka aliyekuwa akisumbuliwa na magonjwa ya moyo ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa kuanzisha matibabu ya moyo nchini kusaidia wagonjwa wa moyo waliopo Tanzania na nchi za jirani. Jane aligundulika kuwa na matatizo ya moyo kupitia kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanywa na wataalam wa afya wa JKCI nchini Malawi mwezi Mei mwaka huu katika hospitali ya Queen Elizabeth. Jane alisema kupitia kambi hiyo tatizo la moyo alilokuwa nalo liliweza kuonekana na kupewa rufaa kufika JKCI kwaajili ya matibabu zaidi, hivyo kufika kwake katika Taasisi hiyo kumemsaidia kupata matibabu kwa haraka, karibu na nchi yake na kupunguza gharama kama angekweenda kutibiwa nje ya Afrika. “Nilipofanyiwa uchunguzi pale Hospitali ya Queen Elizabeth niligundulika kuwa na mapigo ya moyo ya chini ya asilimia 30 hivyo kupewa rufaa kufika JKCI kwa ajili ya matibabu ya kuwekewa kifaa kisaidizi cha moyo (Pacemaker) na kufanya mapigo yangu ya m...
Utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na Viongozi wa Taasisi hiyo wakati wa kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga akiwasilisha utekelezaji wa mpango kazi wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 wakati wa kikao cha viongozi wa Taasisi hiyo kupitia utekelezaji wa bajeti leo jijini Dar es Salaam Afisa Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Deborah Wami akielezea namna kitengo cha Mipango kilivyoweka mikakati ya udhibiti wa bajeti wakati wa kikao cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akichangia mada wakati wa kikao cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 leo katik...
Kwa mara ya kwanza matibabu ya uzibuaji wa mishipa ya damu ya miguu yafanyika nchini
- Get link
- X
- Other Apps
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu hayo inayofanyika jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 100 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu iliyoziba wanatarajia kupatiwa matibabu katika kambi hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka Hospitali ya BLK iliyopo nchini India Suhail Bukhari wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu hayo inayofanyika jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 100 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu iliyoziba wanatarajia kupatiwa matibabu katika kambi hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini. Na: JKCI *****...
Wagonjwa 70 kuzibuliwa mishipa ya damu ya miguu iliyoziba
- Get link
- X
- Other Apps
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao Suhail Bukhari kutoka Hospitali ya BLK iliyopo nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu hayo inayofanyika jijini Dar es Salaam. Jumla ya wagonjwa 70 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu iliyoziba wanatarajia kupatiwa matibabu katika kambi hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini Picha na: JKCI ***********************************************************************************************************
Wafanyakazi wa JKCI wapata mafunzo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa
- Get link
- X
- Other Apps

Mwezeshaji kutoka kampuni ya VERTEX Charles Nduku akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kutoa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia wakati wa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa kada mbalimbali leo katika ukumbi wa JKCI uliopo jijini Dar es Salaam Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma bora kwa wateja wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea kwenye mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Mfanyakazi wa mapokezi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Safina Tibanyendera akichangia mada wakati wa mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma bora kwa wateja yaliyofanyika kwa wafanyakazi wa kada mbalimbali wa taasisi hiyo leo katika ukumbi wa JKCI uliopo jijini Dar es Salaam. Mwezeshaji kutoka kampuni ya VERTEX Charles Nduku akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kutoa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia wakati wa mafunz...