Posts

Showing posts from November, 2024

Gambia kushirikiana na JKCI tiba ya matibabu ya moyo

Image
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwatembeza katika baadhi ya maeneo ya Taasisi hiyo viongozi kutoka  Wizara ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya Gambia walipotembelea taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naiz Majani akiwaelezea namna ambavyo huduma zinatolewa kwa wagonjwa viongozi kutoka  Wizara ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya Gambia walipotembelea taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali leo jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwaonesha moja ya chumba cha VIP viongozi kutoka Wizara ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya nchini Gambia walipotembelea taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona uwekezaji uliowekw...

Wataalamu wa JKCI wapigwa msasa matibabu ya moyo

Image
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia Jayme Bennetts akielezea namna wagonjwa wa upasuaji wa moyo wanatakiwa kuhudumiwa wakati wa mafunzo ya siku moja yanayofanyika leo kwa wataalamu wa OHI na wenzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sunday Mwera akielezea dawa ambazo wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo wanapatiwa leo wakati wa mafunzo ya siku moja yanayofanyika kwa wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia. Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akichangia mada leo wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wataalamu wa JKCI pamoja na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasi...

Bodi ya wadhamini yaipongeza JKCI kwa mafanikio

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Asha Izina wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Balozi Mwanaidi Maajar wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimkabidhi tuzo aliyekuwa mjumbe wa bodi hiyo CPA Godfrey Kilenga wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimpa mkono wa pongezi aliyekuwa mjumbe wa b...

Wafundishwa jinsi ya kurekebisha valvu za moyo

Image
Wataalamu wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia kumfanyia upasuaji wa kurekebisha valvu ya moyo mgonjwa mwenye matatizo ya valvu wakati wa kambi maalumu ya siku 6 inayofanyika katika taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto mwenye tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya siku 6 inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwakushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia. Jumla ya watoto 10 kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo. Na: JKCI ******************************************************************************************************* Wataalamu wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanapewa mafunzo ya kutibu valvu za moyo kwa kuzirekebisha badala ya kuzitoa na kuweka valvu za bandia. Mafunz...

Wasanii waishukuru JKCI kwa kuwapa huduma za matibabu ya moyo

Image
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Kawe Nicholaus Steven akizungumza na mwananchi aliyefika katika kliniki hiyo iliyopo jengo la Mkapa Health Plaza barabara ya Tuari jijini Dar es Salaam kwaajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo. Wananchi waliofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Kawe wakisoma taarifa mbalimbali zinazohusiana na taasisi hiyo wakati wakisubiri kupatiwa huduma. Picha na: Khamis Mussa ************************************************************************************************************** Na Khamisi Mussa - Dar es Salaam Wasanii waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwapa huduma za uchunguzi, matibabu ya moyo pamoja na elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo. Huduma hiyo inafanyika katika Kliniki ya JKCI iliyopo Kawe jengo la Mkapa Hearth Plaza barabara ya Tuari imelenga kuyafikia makundi ya wasanii na wanamichezo kwa kuwapa huduma bila gharama kila jumamosi na jumapili kwa kipin...

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge   pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bruce Mwile wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya JKCI na Benki ya CRDB leo wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam.    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge   pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bruce Mwile wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya JKCI na Benki ya CRDB leo wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam.   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge   pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bruce Mwile wakimjulia hali mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo kabla ya hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano bain...

Dkt. wa JKCI kupewa tuzo kutoka American College of Cardiology - ACC

Image
Chuo cha taaluma ya magonjwa ya moyo (American College of Cardiology – ACC) cha nchini Marekani kutoa tuzo kwa daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai. Tuzo hiyo inatolewa baada ya kamati ya tuzo ya ACC kupokea fursa za wanazuoni za Hani Najm Global ambao huwapa washindi fursa kubadilishana ujuzi na wataalamu wenzao yatakayofanyika katika kliniki ya Clevaland iliyopo Ohio’s. Akizungumzia tuzo hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai alisema mbali na kupewa tuzo hiyo wakati wa mkutano wa ACC utakaofanyika Chicago mwezi Machi mwakani pia atapata fursa ya kushiriki mafunzo ya wiki nne yatakayotolewa katika kliniki ya Clevaland iliyopo Ohio’s nchini Marekani. “Fursa hii hutolewa kila mwaka kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo duniani ambapo mwaka huu tumepata nafasi wataalamu watatu nikiwemo mimi kutoka nchini Tanzania”, alisema Dkt. Khuzeima Dkt. Khuzeima alitoa shukrani zake kwa Chuo ...

JKCI Cycling Club yachangia damu kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa na wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club) pamoja na kikundi cha waendesha baiskeli cha Twende Butiama jana kabla ya klabu ya JKCI cycling kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo pamoja na kuchangia damu. Wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club) pamoja na wenzao wa kikundi cha Twende Butiama wakifanya maandamano ya baiskeli ya umbali wa kilometa 10 kabla ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI pamoja na kuchangia damu. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club) pamoja na kikundi cha waendesha baiskeli cha Twende Butiama jana wakati klabu ya JKCI cycling ilipokuwa ikitoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo pamoja na kuchangia damu. W...

Wagonjwa wa presha watakiwa kuhudhuria kliniki

Image
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKIC) Khairoon Mohamed akizungumza na mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Elikaanaeny Urio akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akimfundisha namna ya kuzingatia lishe bora mwana...