Gambia kushirikiana na JKCI tiba ya matibabu ya moyo
Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naiz Majani akiwaelezea namna ambavyo huduma zinatolewa kwa wagonjwa viongozi kutoka Wizara ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya Gambia walipotembelea taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwaonesha moja ya chumba cha VIP viongozi kutoka Wizara ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya nchini Gambia walipotembelea taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya
nchini Gambia Dkt. Omar Jah akielezea lengo la ujio wa wataalamu kutoka nchini
Gambia walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya
kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali.
Katibu Mkuu kutoka Wizara ya
Jinsia Watoto na Maendeleo ya Jamii nchini Gambia Roheyatou Kah akieleza namna
alivyojifunza wakati ya ziara ya viongozi kutoka Wizara ya Afya na wengine
kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya nchini Gambia walipotembelea Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na
Serikali.
Baadhi ya viongozi kutoka Wizara
ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima ya Afya ya nchini Gambia wakisikiliza
walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kujifunza
na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Afya na wengine kutoka Taasisi ya Bima
ya Afya ya nchini Gambia mara baada ya kutembelea taasisi hiyo leo kwaajili ya
kujifunza na kuona uwekezaji uliowekwa na Serikali.
Picha na: Khamis Mussa
*********************************************************************************************************************************************************************************************
Viongozi 15 wa ngazi ya juu kutoka Serikali ya Gambia wametembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinatolewa na kuangalia namna ambavyo nchi hiyo itashirikiana na JKCI katika matibabu ya moyo.
Viongozi hao waliotembelea taasisi hiyo leo iliyopo jijini
Dar es Salaam ni makatibu wakuu, wenyeviti wa bodi, wakuu wa taasisi
za afya na mamlaka za usimamizi wa afya za nchi hiyo .
Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya nchini
Gambia Dkt. Omar Jah alisema wako nchini kwaajili ya kujifunza mambo ya afya
ikiwemo kuona huduma za matibabu ya kibingwa zinazotolewa pamoja na mifumo ya
TEHAMA jinsi inavyofanya kazi.
Dkt. Jah alisema wameona jinsi Tanzania ilivyofanikiwa katika mfumo wa bima ya afya wamejifunza katika mifumo na kuona inavyofanya
kazi pia wameona jinsi ambavyo huduma za kibingwa
za matibabu mbalimbali zinavyotolewa
“Wenzetu hawa wa JKCI wako mbele katika tiba ya moyo tumekuja
hapa ili kuona namna gani tutashirikiana
nao ili wawatume madaktari wao nchini kwetu kutoa huduma,tuwalete wanafunzi wetu
waje kujifunza jinsi ya kutibu magonjwa ya moyo pamoja na kuwaleta wagonjwa
wetu waje kutibiwa hapa kuliko kuwapeleka nje ya Afrika.
“Ushirikiano baina ya nchi za Afrika ni mzuri kwani ni rahisi
na unaimarisha mahusiano kati ya nchi moja na nyingine tumejifunza vitu vingi hivyo basi ninawaomba wataalamu
wa afya wa Tanzania waje kutembelea
nchini kwetu naamini nao watajifunza kitu”, alisema Dkt. Jah.
Kwa upande
wake Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.Delilah
Kimambo aliishukuru serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioifanya ya kuwekeza katika sekta ya afya hasa katika Taasisi hiyo
jambo lililosababisha nchi nyingi kwenda kujifunza namna wanavyotoa huduma za matibabu ya moyo pamoja na mafunzo
wanayoyatoa.
“Leo hii tumepokea ugeni wa viongozi 15 kutoka nchini Gambia ambao
wamekuja kujifunza katika Taasisi yetu, tunaona faraja na furaha kuona nchi zingine zinakuja
kujifunza Tanzania kuona namna ambavyo
serikali ilivyowekeza katika matibabu ya moyo pamoja na kuona kazi kubwa
inayofanywa na wataalamu wetu”, alisema Dkt. Delilah.
Comments
Post a Comment