JKCI yatoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samuel Rweyemamu akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wahariri  unaofanyika jijini Dar es Salaam.


Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samuel Rweyemamu akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wahariri unaofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa JKCI Anna Nkinda.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akiishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwatuma wataalamu wake kwenda kutoa elimu pamoja na kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wao wa mwaka unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu kambi maalumu za matibabu ya moyo zinazofanywa na taasisi hiyo wakati wa mkutano wa mwaka wa wahariri unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu kambi maalumu za matibabu ya moyo zinazofanywa na taasisi hiyo wakati wa mkutano wa mwaka wa wahariri unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Picha na Khamis Mussa

***************************************************************************************************************************************************************************************************

Wahariri wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kuchukuwa hatua katika kupambana na magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na kula vyakula bora, kufanya mazoezi na kutokunywa pombe kupitiliza.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samuel Rweyemamu wakati akitoa elimu ya magonjwa ya moyo katika mkutano mkuu wa mwaka wa wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Dkt. Rweyemamu alizitaja sababu zingine zinazosababisha  magonjwa ya moyo  ni pamoja na  matumizi ya bidhaa aina ya tumbaku, changamoto za maisha zinazosababisha msongo wa mawazo na mgonjwa kurithi tatizo hilo.

“Ninawaomba mchukuwe hatua ili muweze kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo kwani magonjwa haya ambayo matibabu yake ni ya gharama kubwa unaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu”,alisema Dkt. Rweyemamu.

Alizitaja dalili za ugonjwa wa moyo kuwa ni pamoja na kifua kuuma, kubanwa na pumzi, ongezeko la mapigo ya moyo, ukitembea kidogo unachoka, miguu na tumbo kuvimba, kichomi kwenye kifua kwa upande wa kushoto, miguu kujaa, kukosa pumzi, kukohoa kifua kikavu, ganzi mwili mzima, kichwa kuuma na kusikia kizunguzungu.

Dkt. Rweyemamu alisema endapo mtu atapata magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo asiache kutumia dawa atakazoandikiwa na mtaalamu wa afya kwani tiba ya magonjwa hayo ni endelevu na endapo mgonjwa ataacha kutumia dawa anaweza kupoteza maisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile aliishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwatuma wataalamu wake katika mkutano huo kwenda kutoa elimu pamoja na kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo.   

“Ninawashukuru kwa elimu mliyoitoa ninaomba ushirikiano huu uwe endelevu,  tutakuwa mabalozi wa kuwaambia watu wapime afya zao kwani watu wengi wakifikia umri wa kufanikiwa ndipo changamoto za kiafya zinaanza”.

 “Taasisi hii ilitupa nafasi ya kupima afya ya moyo na kutibiwa bila malipo katika kliniki yao ya Kawe  leo hii wamekuja kutupa elimu na kwa ambao hawakupata nafasi ya kupima Kawe wamefuatwa na kupimwa afya zao hapa,  ninawaomba muendelee na moyo wenu huohuo wa kujitoa kwaajili ya wengine”, alisema Balile.

Balile alisema ni jambo la kujivunia kuona Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa watanzania na wasio watanzania kuna wagonjwa wanakwenda kutibiwa JKCI kutoa nchi mbalimbali zikiwemo za Rwanda, Burundi, Somalia, Malawi, Comoro, Zambia,Msumbiji,  Kenya na Congo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Taasisi hiyo Anna Nkinda aliwashukuru wahariri hao kwa kufanya kazi na JKCI ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu magonjwa ya moyo.

Anna alisema ili kusogeza kwa ukaribu zaidi huduma za kibingwa za matibabu ya moyo JKCI ilianzisha  huduma ya tiba mkoba ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan outreach services kwa kufanya kambi maalumu za uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi.

"Gharama za matibabu ya moyo ni kubwa ninawaomba tunapotangaza kuwa na kambi za matibabu ya moyo kwa wananchi mtusaidie kutoa taarifa ili watu wengi wafahamu na kwenda kupima afya za mioyo yao mapema kuliko kusubiri wakati wameanza kuumwa", alisema Anna.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024