JKCI yawafikia washirika wa KKKT Wazo hill
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) George Longopa akimsikiliza mwananchi aliyefika kwaajili ya
kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tatu ya
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na JKCI katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Wazo Hill jijini Dar es
Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali
ya Dar Group Fatma Suedy akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyefika
kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya
siku tatu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na JKCI
katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Wazo Hill
jijini Dar es Salaam.
Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Devotha Mapunda akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa
umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG) mwananchi aliyefika kwaajili ya
kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tatu ya
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na JKCI katika Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sigfrid
Shayo akipima mapigo ya moyo ya mwananchi aliyefika kwaajili ya kufanyiwa
uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tatu ya Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na JKCI katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania – KKKT DMP Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Na: JKCI
****************************************************************************************************************
Waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
usharika wa Wazo Hill wameishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
kuwakumbuka wakazi wa Kata ya Wazo na kuwafikishia huduma ya uchunguzi na
matibabu ya magonjwa ya moyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kambi maalumu ya
siku tatu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba wamesema kuwa huduma za
kibingwa kuwafuata katika Kata ya Wazo Tegeta haijawahi kutokea kwani hii
imekuwa mara ya kwanza.
Jackson Msongole alisema Kanisa la Kiinjili la Kiluther (KKKT)
usharika wa Wazo Hill limetoa msaada mkubwa kuruhusu huduma za uchunguzi kwa
wananchi wa Wazo Tegeta kupata huduma za kibingwa kwani wapo ambao hawawezi
kuzifuata huduma hizo mahali zilipo.
“Watanzania hatuna tabia ya kufanya uchunguzi wa afya,
kwasababu hiyo wengi wetu leo hatuwezi kuzifuata huduma hizi mahali zilipo
lakini zikitufikia kama hivi zinatupa motisha ya kufanya uchunguzi wa afya”,
alisema Jackson
Jackson alisema JKCI imewapa mwanga wananchi kuwa wanafanya
uchunguzi wa afya kabla ya kuumwa kwani inawawezesha kujua hali za afya yao na
kuishi maisha ambayo yatawasaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Naye muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)
usharika wa Wazo Hill Grace Hangwa amewapongeza wataalamu wa JKCI kwakuwa na
ujuzi wa hali ya juu kuwawezesha wananchi kuyafanya magonjwa ya moyo na namna
ya kujikinga na magonjwa hayo.
“Kwakweli kupitia kambi hii nimejifunza vitu vingi sana,
tumekuwa tukiishi bila ya kujali afya zetu kwa kutumia vitu ambavyo vinaweza
kutuharibia afya zetu lakini leo nimepata somo zuri kutoka kwa wataalamu wa
JKCI”, alisema Grace
Grace alisema wataalamu waliosomea masuala ya afya wanatakiwa
kuifuta jamii mara kwa mara kuielimisha kuhusu lishe bora pamoja na namna ya
kuwa na matumizi mazuri ya mchanganyiko wa vyakula.
Aidha waumini hao wameiomba Serikali kuendelea kuwekeza
katika matibabu ya kibingwa nchini kuwasaidia wananchi wake kupata huduma bora
nyumbani na kuacha kuzifuata huduma hizo nje ya nchi.
Comments
Post a Comment