Wataalamu wa Rediolojia wa JKCI kuendelea kulinda afya za wagonjwa
Wataalamu wanaotoa huduma za rediolojia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakikata keki wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akizungumza na wataalamu wa rediolojia
wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo
tarehe 8 mwezi Novemba.
Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akielezea namna huduma za upasuaji mdogo wa moyo unavyotumia mionzi wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba.
Mkuu wa Kitengo cha Rediolojia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Praygod Lekasio akiwapongeza wataalamu wa rediolojia kwa kutoa
huduma nzuri kwa wagonjwa wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani
inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba.
Baadhi ya wataalamu wa rediolojia wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya rediolojia
duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba.
Na: JKCI
********************************************************************************************************************************
Wataalamu wa Rediolojia wanaofanya kazi Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufuata taratibu wakati wa kutoa huduma na
kulinda afya za wagonjwa wanaowahudumia.
Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Rediolojia wa
JKCI Dkt. Praygod Lekasio wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duninai
inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba.
Dkt. Praygod ambaye pia ni daktari bingwa mbobezi wa rediolojia
alisema mwaka 2011 taasisi tatu za Amerika kusini, Amerika na Europe waliweza kukutana
na kuadhimisha siku ya radiolojia kutokana na umuhimu wake katika kuboresha
huduma za matibabu kwa wagonjwa.
“Sisi kama JKCI ni sehemu ya dunia kwani tunaona ujio na ugunduzi
wa rediolojia umeweza kuboresha afya kwa wagonjwa wetu katika kutatua na
kuyatibu magonjwa ya moyo”,
Dkt. Praygod alisema ujio wa Rediolojia umesaidia katika
kufanyika kwa upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo na kuwapunguzia
wagonjwa muda wa kukaa wodini kutokana na vidonda vya upasuaji huu kupona
mapema.
“Miaka ya nyuma watoto wenye matatizo ya moyo waliokuwa
wakitibiwa JKCI ilikuwa ngumu kuwafanyia upasuaji mdogo wa moyo lakini kutokana
na ugunduzi wa radioloji sasa tunawafanyia watoto upasuaji wa moyo kupitia
tundu dogo lililopo kwenye paja”, alisema Dkt. Praygod
Kwa upande wake daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. George Longopa alisema mafanikio makubwa ya JKCI
yamechangiwa na utoaji wa huduma za rediolojia.
Dkt. Longopa alisema huduma ya rediolojia inatumika kuongoza
wakati wa kufanya vipimo vikubwa ikiwemo X-ray lakini kwa JKCI huduma hiyo
imekuwa ikitumika pia wakati wa kufanya upasuaji mdogo wa moyo kwa kutumia
mtambo wa cathlab.
“Mionzi inayotumika kutoa huduma kwa wagonjwa imekadiriwa kulingana
na kiasi kinachohitajika kwa wakati husika hivyo haiwezi kuleta madhara katika
mwili wa binadamu”, alisema Dkt. Longopa
Comments
Post a Comment