Bodi ya wadhamini yaipongeza JKCI kwa mafanikio
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Asha Izina wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya
Taasisi hiyo Balozi Mwanaidi Maajar wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo
kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimkabidhi tuzo aliyekuwa mjumbe wa bodi hiyo CPA Godfrey Kilenga wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimpa mkono wa pongezi aliyekuwa mjumbe wa bodi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimkabidhi tuzo aliyekuwa mjumbe wa bodi
hiyo Adv. Haruni Matagane wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo
kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimkabidhi tuzo aliyekuwa mjumbe wa bodi
hiyo Abdulmalick Mollel wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika
hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
hiyo Dkt. Peter Kisenge
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akitoa neno la shukrani kwa viongozi wa
Taasisi hiyo wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipngo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akitoa taarifa ya fedha za taasisi hiyo wakati wa
kikao cha mwisho cha Bodi ya Wadhamini wa JKCI kilichofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto na mwenyekiti
wa kamati ya kuratibu fedha zinazotolewa kwaajili ya matibabu ya watoto
Naizhijwa Majani akitoa taarifa ya fedha zilizokusanywa kwenye hafla ya gala
dinner wakati wa kikao cha mwisho cha Bodi ya Wadhamini wa JKCI kilichofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam.
Na: JKCI
*************************************************************************************************
Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
iliyomaliza muda wake yajivunia kufanya kazi vizuri na uongozi wa Taasisi hiyo
kuifanya kutambulika kimataifa.
Akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha bodi hiyo
kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa
Bodi hiyo Asha Izina alisema mafanikio yaliyopo JKCI yanatokana na ushirikiano
mzuri uliopo pamoja na kujitoa kwa viongozi na wafanyakazi wote.
Asha alisema menejimenti ya JKCI imekuwa na hari ya kufikia
malengo waliyojiwekea ili iweze kuwa tofauti na wengine jambo ambalo
limefanikiwa kwa asilimia 100.
“Leo tunasimama tunajivunia kwa kipindi cha miaka mitatu
tumeweza kufanya kazi nzuri katika taasisi hii na kuitambulisha ndani na nje ya
nchi lakini pia tumeiweka katika hadhi yakimataifa”, alisema Asha.
Asha amewataka wafanyakazi wa Taasisi hiyo kuendelea kuwa na
ushirikiano kwani bodi hiyo inaondoka ikiwa na matumaini ya kuendelea kuiona
JKCI ikikuwa zaidi na isirudi nyuma.
“Bodi inawashukuru kwa ushirikiano mliokuwa nao twetu kwani
hatujapata changamoto kufanya kazi na nyie, pale tulipokuwa tukikumbushana ilikuwa
ni kwaajili ya kujenga na kuleta mafanikio katika taasisi yetu”, alisema Asha
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema bodi hiyo imeleta mageuzi makubwa
katika taasisi hiyo ambayo yameongeza weledi na mafanikio kwa nchi.
“Nimekuwa nikiiona taasisi hii tangu ilivyoanzishwa mwaka
2015, kwakweli ilipofikia sasa ni hatua kubwa sana imepiga na hii inatokana na ushirikiano
uliopo kati ya Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wote”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge aliishukuru bodi ya wadhamini inayomaliza muda
wake kwa kuwa na maono ambayo yameifanya taasisi hiyo kupiga hatua na kuweza
kuongeza huduma za kibingwa bobezi kutolewa hapa nchini.
“Mnaweza msiyaone mafanikio tuliyofikia lakini waliopo nje
wanatupongeza sana kwa hatua hii kubwa tuliyopo sasa hii yote inatokana na
uongozi mzuri uliopo baina yetu”,
“Bodi hii ilivyoanza tulikuwa na tawi moja la Upanga lakini
leo mnamaliza muda wenu tukiwa na matawi matatu ambayo ni Dar Group, Kawe na
Oyster bay ambalo litafunguliwa wakati wowote mwezi ujao, nawashukuru sana”
Naye mjumbe wa bodi hiyo inayomaliza muda wake CPA Godfrey Kilenga
aliwashukuru wajumbe wa bodi na menejimenti ya JKCI kwa ushirikiano
waliouonyesha kupelekea kupata fursa mbalimbali za kuijenga na kuikuza.
CPA Kilenga alisema Taasisi ikifanya vizuri safa uenda kwa
kila mtu na ikitokea ikafanya vibaya sifa mbaya zitaenda kwa kila mtu hivyo wao
wanajivunia kuona wanapata sifa nzuri kutoka kwa wadau wa afya nchini.
“Ninahakika bodi mpya itakayokuja nayo mtaipa ushirikiano na
kuweza kufanya nayo kazi vizuri, hii yote ni kwaajili ya kuijenga Tanzania yetu
na kuifanya dunia kutujua katika sekta hii ya kutoa huduma za kibingwa za
matibabu ya moyo”, alisema CPA Kilenga.
Comments
Post a Comment