Shirika la Save a Childs Heart laipa JKCI kifaa cha kupima moyo chenye thamani ya shilingi Milioni 200
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipokea kifaa kinachotumika kupima moyo (Transesophageal
Echocardiography (TEE) probe) kwa watoto chenye thamani ya shilingi milioni 200
kilichotolewa na wataalamu wa afya kutoka Shirika la Save a Childs Heart lililopo
nchini Israel wakati wa harambee ya kuchangia matibabu ya watoto iliyofanyika
katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi
bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto.
Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka shirika la Save a Childs Heart lililopo nchini
Israel wakimfanyia mtoto upasuaji wa
kuziba tundu lililopo kwenye kupitia mtambo wa cathlab wakati wa kambi maalumu
iliyomalizika hivi karibuni. Jumla ya watoto 19 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa
moyo.
Picha na: JKCI
********************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment