JKCI Cycling Club yachangia damu kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa na wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club) pamoja na kikundi cha waendesha baiskeli cha Twende Butiama jana kabla ya klabu ya JKCI cycling kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo pamoja na kuchangia damu.
Wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club)
pamoja na wenzao wa kikundi cha Twende Butiama wakifanya maandamano ya baiskeli
ya umbali wa kilometa 10 kabla ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya
watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI pamoja na kuchangia damu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli
(JKCI cycling club) pamoja na kikundi cha waendesha baiskeli cha Twende Butiama
jana wakati klabu ya JKCI cycling ilipokuwa ikitoa msaada wa vitu mbalimbali
kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo pamoja na kuchangia damu.
Wanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club)
wakitoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo
wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana jijini Dar es
Salaam.
Wananchama wa klabu ya kuendesha baiskeli (JKCI cycling club)
wakichangia damu kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana baada ya kutoa msaada wa mahitaji
mbalimbali kwa watoto hao.
Picha na: Hamis Mussa
***************************************************************************************************
Na Hamisi Mussa- Dar es Salaam
Klabu ya kuendesha baiskeli ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI Cycling club) imepongezwa kwa kuwakumbuka watoto wenye magonjwa ya moyo
kwa kuwachangia damu pamoja na kuwapa zawadi za mahitaji mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipokutana na kikundi
hicho kabla ya kutoa zawadi na kuwataka kuendelea kuhamasisha michezo katika
jamii ili waweze kijikinga na magonjwa ya moyo.
“Mmefanya ubunifu mkubwa kuanzisha klabu hii ya kuendesha
baiskeli hapa JKCI, uongozi wa Taasisi unaungana nanyi kuhakikisha hiki
mlichokianzisha kinakuwa kikubwa na kuhusisha wadau mbalimbali”, alisema Dkt.
Kisenge
Dkt. Kisenge alisema kuendesha baiskeli ni sehemu ya michezo na
michezo huchangia kuimarisha afya, jamii ikibuni vikundi mbalimbali vya michezo
kama ambavyo JKCI inafanya itasaidia kupunguza magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo
magonjwa ya moyo
“Nawashukuru sana kwakuweza kuwakumbuka watoto wetu
wanaotibiwa JKCI kwa kujitoa kuchangia damu pamoja na kuwapa mahitaji mbalimbali
ambayo ni ya muhimu kwao”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake mwanachama wa klabu ya kuendesha baiskeli
(JKCI Cycling Club) Henry Magwaza alisema klabu hiyo imeungana na klabu
mbalimbali kuendesha baiskeli kwa pamoja na kushiriki kuchangia damu kwaajili
ya watoto wanaotibiwa JKCI.
“Klabu ya kuendesha baiskeli ya JKCI (JKCI Cycling Club) tumeweza
kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya watoto wenye magonjwa ya moyo waliolazwa
katika Taasisi hii tukiwa na lengo la kuonyesha upendo kwao”, alisema Henry
Henry alisema klabu hiyo imeamua kufanya matendo ya huruma
kwa watoto hao kwani wamekuwa wakikaa wodini kwa muda mrefu na hivyo kuwa
wapweke kutokana na maisha wanayopitia.
Comments
Post a Comment