Dkt. wa JKCI kupewa tuzo kutoka American College of Cardiology - ACC


Chuo cha taaluma ya magonjwa ya moyo (American College of Cardiology – ACC) cha nchini Marekani kutoa tuzo kwa daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai.

Tuzo hiyo inatolewa baada ya kamati ya tuzo ya ACC kupokea fursa za wanazuoni za Hani Najm Global ambao huwapa washindi fursa kubadilishana ujuzi na wataalamu wenzao yatakayofanyika katika kliniki ya Clevaland iliyopo Ohio’s.

Akizungumzia tuzo hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai alisema mbali na kupewa tuzo hiyo wakati wa mkutano wa ACC utakaofanyika Chicago mwezi Machi mwakani pia atapata fursa ya kushiriki mafunzo ya wiki nne yatakayotolewa katika kliniki ya Clevaland iliyopo Ohio’s nchini Marekani.

“Fursa hii hutolewa kila mwaka kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo duniani ambapo mwaka huu tumepata nafasi wataalamu watatu nikiwemo mimi kutoka nchini Tanzania”, alisema Dkt. Khuzeima

Dkt. Khuzeima alitoa shukrani zake kwa Chuo cha taaluma ya magonjwa ya moyo (American College of Cardiology – ACC) kwa kumpa nafasi hiyo ambayo inaenda kumuongezea utaalamu zaidi katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo.

********************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)