Bilion 4.1 zakusanywa kugharamia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa tuzo mwakilishi kutoka Benki ya CRDB ya kutambua mchango wao katika kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa harambee ya kuchangia matibabu ya watoto iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha aliyomtembelea mtoto wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa moyo nchini iliyotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila wakati wa harambee ya kuchangia matibabu ya watoto iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hudi ya shilingi milioni 100.1 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) Elirehema Maturo mchango uliotolewa na kamuni hiyo kwaajili ya kugharamia matibabu ya moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana wakati wa harambee ya kuchangia matibabu ya watoto iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto.
Comments
Post a Comment