Wataalamu wa JKCI wapigwa msasa matibabu ya moyo



Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia Jayme Bennetts akielezea namna wagonjwa wa upasuaji wa moyo wanatakiwa kuhudumiwa wakati wa mafunzo ya siku moja yanayofanyika leo kwa wataalamu wa OHI na wenzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sunday Mwera akielezea dawa ambazo wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo wanapatiwa leo wakati wa mafunzo ya siku moja yanayofanyika kwa wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia.

Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akichangia mada leo wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wataalamu wa JKCI pamoja na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ramadhani Hamis akichangia mada leo wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wataalamu wa JKCI pamoja na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia Darren Wolfers akichangia mada leo wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia.



Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakisikiliza wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wataalamu hao yanayofanyika katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na: JKCI

*********************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)