Wagonjwa wa presha watakiwa kuhudhuria kliniki
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKIC) Khairoon Mohamed akizungumza na mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Elikaanaeny Urio akimpima kipimo cha kuangalia jinsi
moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi aliyefika katika
kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)
usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu
276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna
Faraji akimfundisha namna ya kuzingatia lishe bora mwananchi aliyefika katika
kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)
usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu
276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Mtaalamu wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Kennedy Hemely akimpima wingi wa sukari kwenye damu mtoto aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Zabella Mkojera akimuuliza maswali ya ufahamu mwananchi aliyefika katika kambi
maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba
mkoba iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)
usharika wa Wazo Hill na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu
276 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Na: JKCI
***********************************************************************************************************
Wagonjwa waliogundulika kuwa na tatizo la shinikizo la juu la
damu (Presha) wametakiwa kuendelea kuudhuria kliniki kupata muendelezo wa elimu
kuhusu ugonjwa huo pamoja na kutumia dawa kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa
afya.
Wito huo umetolewa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Elikaanaeny Urio wakati wa kuhitimisha
kambi maalumu ya siku tatu ya matibabu ya moyo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)
usharika wa Wazo na kumalizika jana jijini Dar es Salaam.
Dkt. Urio alisema mwitikio katika kambi hiyo umekuwa mkubwa
ambapo idadi kubwa ya watu wamekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu,
huku wengine wakiwa na magonjwa ya sukari na matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo
ambao unafanya kazi chini ya kiwango.
“Watu tuliowakuta na tatizo la shinikizo la juu la damu wapo
ambao wamegundulika hivi karibuni na wengine wamegendulika siku nyingi lakini
hawakuwa na ufahamu vizuri wa namna gani watumie dawa kwani wapo waliotumia
dawa kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuacha kutumia wakiamini wamepona”, alisema
Dkt. Urio.
Dkt. Urio alisema Jamii inapaswa kuwa na tabia ya kupima mara
kwa mara kwani tatizo la shinikizo la juu la damu mara nyingi linaweza
lisionyeshe dalili hivyo kusababisha matatizo mengine yanayoendana na tatizo
hilo.
Kwa upande wake daktari wa watoto kutoka JKCI Hospitali ya
Dar Group Gloriamaria Kunambi alisema katika kambi hiyo wamewakuta watoto 11
wana matatizo ya moyo ambayo hayakuwahi kugundulika kabla hivyo kuwapa rufaa
kufika JKCI kwaajili ya matibabu zaidi.
Dkt. Gloriamaria alisema kambi hiyo imekuwa na manufaa
kwasababu wazazi wa watoto waliofika katika kambi hiyo wamepata uelewa wa
magonjwa ya moyo pamoja na dalili zake uelewa ambao utawawezesha kuwalinda
watoto wao wasipate magonjwa hayo.
“Wazazi wengi walikuwa hawajui dalili za magonjwa ya moyo kwa
watoto, hii inaonyesha kuna watoto wapo majumbani wana shida za moyo lakini
wazazi wao kutokana na kutokuwa na uelewa wanakosa fursa kama hizi za kufanyiwa
uchunguzi na matibabu ya moyo”, alisema Dkt. Gloriamaria
Naye afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna
Faraji alisema tatizo la uzito mkubwa limekuwa likiwakabili watu wengi kwani
kupitia kambi hiyo pia limeonekana kuchukua nafasi kubwa kwa watu wengi.
Husna alisema uelewa wa masuala ya lishe katika jamii bado
upo chini kwani kumekuwa na matumizi mengi ya vilevi, matumizi ya chumvi
nyingi, matumizi makubwa ya sukari na matumizi ya vinywaji vyenye sukari nyingi
na vilivyosindikwa.
“Vitu vyote nilivyovitaja hapo vikitumika kwa wingi
vinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzito, tumetoa elimu inayohusu mlo
kamili uliohusisha makundi yote ya chakula pamoja na kuzingatia njia za
upishi”, alisema Husna.
Husna alisema suala la mlo kamili bado nichangamoto katika
jamii kwani watu wengi wanatumia vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa hivyo
kuwaelekeza kuzingatia vyakula visivyo na mafuta mengi na matumizi makubwa ya
mboga za majani na matunda.
Katika kambi hiyo jumla ya 276 wamefanyiwa uchunguzi wa
magonjwa ya moyo kati yao watoto wakiwa 50 ambapo watu wazima 46 na watoto 35
wamepewa rufaa kufika JKCI kwaajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Comments
Post a Comment