Shilingi bilioni 500 zaokolewa matibabu ya moyo kufanyika nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mtendaji Mkuu wa Taasisi
isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa
Majani wakifurahia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kuchangisha
fedha kwaajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo ijulikanayo “Kutoa
ni Moyo” leo katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wadau
wakati wa hafla fupi ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya kuchangisha fedha kwaajili
ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo ijulikanayo “Kutoa ni Moyo”
inayofanywa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation
(HTAF).
Mtendaji Mkuu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa Majani akitoa taarifa ya fedha zilizokusanywa na Taasisi hiyo kusaidia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa hafla fupi ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya kuchangisha fedha kwaajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo ijulikanayo “Kutoa ni Moyo” leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
**********************************************************************************************
Serikali kupitia
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni
500 fedha ambazo zingetumiwa na Serikali kupeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa nje
ya nchi.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo kuzindua
kampeni ya kitaifa ya kuchangisha fedha kwaajili ya matibabu ya watoto wenye
magonjwa ya moyo ijulikanayo “Kutoa ni Moyo” inayofanywa na Taasisi isiyo ya
Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF).
Dkt. Kisenge alisema
JKCI imeshawafanyia upasuaji wa moyo watoto 3,500 lakini bado uhitaji ni mkubwa
kwani wapo watoto zaidi ya 1,500 wanasubiria kufanyiwa upasuaji wa moyo ambao
unagharimu kiasi cha shilingi milioni nane hadi 15 kwa mtoto mmoja.
“Tangu Taasisi hii
imeanzishwa kumekuwa na mabadiliko makubwa katika masuala ya tiba ya moyo na
upasuaji wa moyo, JKCI sasa hivi inafanya upasuaji wa moyo wa aina mbalimbali,
kupitia uwekezaji uliofanywa na Serikali sasa hivi alisilia 97 ya magonjwa ya
moyo kwa watoto yanafanyiwa upasuaji katika Taasisi yetu”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema nia
ya JKCI ni kuhakikisha kuwa hamna mtoto yoyote ambaye anatoka katika familia masikini
anapata changamoto ya matibabu ya moyo, kwani JKCI kwa kushirikiana na HTAF
wameweka mikakati ya kuhakikisha watoto hao wanapata matibabu na dawa
kuhakikisha kuwa wanajenga taifa la kesho lililo na afya njema.
“Namshukuru sana Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyotoa fedha nyingi kugharamaia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo, amekuwa akigharamia zaidi ya alisimia 70 ya matibabu ya watoto hao”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge alisema kupitia
kapeni ya kitaifa ya Kutoa ni Moyo inayofanywa na HTAF, JKCI inatamani kuona
kila mtanzania mwenye uwezo anachangia matibabu ya watoto wanaotoka katika
familia duni na kuwapa furaha watoto hao kwani kutoa ni moyo na wakitoa kwa
moyo mmoja watajenga taifa lijalo.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa Majani
alisema watoto 405 wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI wameweza kupatiwa
matibabu kupitia mfuko wa HTAF.
Dkt. Naizihijwa alisema
kupitia gala dinner iliyofanywa na Taasisi hiyo shilingi bilioni 2.7
zilikusanywa kutoka kwa wadau na baadaye kuendelea kukusanya ambapo hadi sasa
jumla ya shilingi bilioni 3.3 zimekusanywa na Taasisi hiyo kugharamia matibabu
ya watoto wenye magonjwa ya moyo.
“Tunatoa shukrani za
dhati kwa wadau wote waliotuunga mkoni katika gala dinner iliyofanyika mwaka
2024, tulipata mshikamano mkubwa kutoka kwa watanzania, taasisi, makampuni,
wafanyabiashara, na marafiki wa watoto wenye magonjwa ya moyo ambao kila mmoja
aliweka mkono wake kufanikisha matibabu ya watoto hao”, alisema Dkt. Naizihijwa
Dkt Naizihijwa alisema
nyuma ya kila mchango kuna maisha ya mtoto, kuna furaha ya familia na tumaini
jipya la kesho, watoto wengi wenye magonjwa ya moyo kama hawatafanyiwa upasuaji
mapema wanaweza wasisherehekee siku yao ya kuzaliwa ya mwaka mmoja na wengine
wengi watashindwa kusherehekea siku yao ya kuzaliwa wakiwa na miaka mitano
lakini wanapohudumiwa mapema maisha yao hubadilika kabisa na kupona.
Dkt. Naizihijwa
aliongeza kuwa mahitaji bado ni makubwa, kila mwaka wanazaliwa watoto takribani
elfu 16 wenye matatizo ya moyo hapa nchini ambapo karibu watoto 4,000 huitaji
matibabu na upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yao.
“Kupitia HTAF
tunaendelea kushirikiana na JKCI kuhakikisha watoto wengi zaidi wanapata nafasi
ya kuishi, kusoma, kucheza, na kutimiza ndoto zao, ndio maana leo tunazindua
rasmi kampeni yetu ya kitaifa ya Kutoa ni Moyo kuhamasisha watanzania wote wanashiriki
kusaidia watoto hawa kupata matibabu yao kwa wakati”, alisema Dkt. Naizihijwa




Comments
Post a Comment