Mhe. Dkt. Kikwete apokea taarifa ya utekelezaji wa fedha za Gala Dinner za matibabu ya moyo kwa watoto


Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge pamoja na Mtendaji Mkuu wa Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa Majani walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni kwa lengo la kumpa taarifa ya utekelezaji wa fedha zilizokusanywa kupitia Gala Dinner ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge mara baada ya kupokea taarifa ya fedha zilizokusanywa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) kupitia Gala Dinner ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI.

Mtendaji Mkuu wa Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa Majani akitoa taarifa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu utekelezaji wa fedha zilizokusanywa kupitia Gala Dinner ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo iliyoandaliwa na HTAF.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni kwaajili ya kumpa taarifa ya utekelezaji wa fedha zilizokusanywa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) kupitia Gala Dinner ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI.

Na JKCI

**********************************************************************************************************

 

Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi