JKCI yawataka wananchi kufanya uchunguzi wa afya, kujua namba zao
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna
akimuelezea huduma za upasuaji wa moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo Rais wa
Shirikisho la Vyama vya Kinywa na Meno Duniani (FDI) Prof. Dkt. Nikolai Sharkov
alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya kimataifa ya vifaa
tiba na huduma za kinywa na meno (Dental Expo 2026) yanayofanyika katika
viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimuelezea mkazi wa Tabata Mussa Mrisho namna betri ya moyo (Pace maker) inavyofanya kazi alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa waonesho ya kimataifa ya vifaa tiba na huduma za kinywa na meno (Dental Expo 2026) yanayofanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akitoa elimu ya ‘Jua Namba Zako’ kwa
baadhi ya washiriki wa waonesho ya kimataifa ya vifaa tiba na huduma za kinywa
na meno (Dental Expo 2026) yanayofanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini
Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimuonesha moja ya kifaa
kinachotumika kuzibua mishipa ya moyo (Stent) Afisa Uhusiano na Masoko wa Prime
your digital partner Eliwaja Peter alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati
wa maonesho ya kimataifa ya vifaa tiba na huduma za kinywa na meno (Dental Expo
2026) yanayofanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Na JKCI
*********************************************************************************************************
Wananchi wametakiwa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara kufahamu hali zao kiafya ili waweze kuepukana na vifo vya gafla vinavyoendelea kukijitokeza katika jamii.
Hayo yalisemwa na Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna wakati wa maonesho
ya Dental Expo yanayofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
Edna alisema kutokana na
ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza JKCI imeanzisha kampeni ya “Jua Namba
Zako” yenye lengo la kuwasaidia wananchi kufahamu viwango muhimu vya afya
vinavyoonesha namna miili yao inavyofanya kazi.
“Tunaposema Jua Namba Zako
tunamaanisha mwananchi anatakiwa kufahamu shinikizo la damu ambalo linapaswa
kuwa 120/80, mapigo ya moyo 60 hadi 100 kwa dakika, kiwango cha sukari kwenye
damu 5.2, Uwiano wa uzito na urefu (BMI) pamoja na kiwango cha mafuta kwenye
damu”, alisema Edna.
Akizungumzia uhusiano
uliopo kati ya magonjwa ya moyo na afya ya kinywa na meno Edna alisema ni
muhimu kwa wagonjwa wa moyo kulinda afya ya kinywa ambayo mara nyingi uwasaidia
wagonjwa kupona haraka wanapofanyiwa upasuaji wa moyo.
“Maonesho haya ni muhimu
kwetu kama JKCI kwani mgonjwa anayetarajia kufanyiwa upasuaji wa moyo lazima afanyiwe
uchunguzi wa afya ya kinywa kabla ya upasuaji kwasababu bakteria wanaoshambulia
meno wanaweza kuhatarisha maisha yake”, alisema Edna.
Kwa upande wao wananchi
waliofika katika banda la JKCI waliishukuru Taasisi hiyo kwa kutoa elimu ya
namna ya kujikinga na magonjwa yasiombukiza kwani wamepata nafasi ya kuelewa kwa
kina umuhimu wa kujua namba zao tano za afya.
“Sisi vijana wa rika hili
ambalo tunatambulika kama Gez tumepata nafasi ya kuzifahamu namba hizi tano za
afya, kupitia elimu hii tutachukua tahadhari ili kuishi maisha marefu”, alisema
Eliwaja Peter Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka Prime.
“Nimefika katika banda la
JKCI na kufaidika na elimu inayotolewa kuhusu uhusiano wa afya ya kinywa na
magonjwa ya moyo, leo nimeweza kupata uelewa kuwa yapo magonjwa ya moyo yanayoweza
kusababishwa na magonjwa ya kinywa endapo hayatatibiwa na kupona”, alisema
Mussa Mrisho Mkazi wa Tabata Bima.




Comments
Post a Comment