Gavana wa Mkoa wa Khomas nchini Namibia atembelea JKCI Kliniki ya Kariakoo


Gavana wa Mkoa wa Khomas nchini Namibia Mhe. Sam Shafiishuna Nujoma akitembelea maeneo ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Kariakoo alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo kuona huduma zinazotolewa.

Na JKCI

***************************************************************************************************

Gavana wa Mkoa wa Khomas nchini Namibia, Mhe. Sam Shafiishuna Nujoma amefanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Kariakoo kuona huduma zinazotolewa na kuangalia namna wananchi wa jimbo hilo watakavyoweza kupata huduma katika Taasisi hiyo.

Ziara hiyo imefanyika leo ambapo Mhe. Nujoma ameweza kuona vifaa vya kisasa vilivyowekezwa na Serikali katika kuboresha huduma bingwa bobezi za matibabu ya moyo nchini Tanzania.

Mhe. Nujoma alisema kusogezwa kwa huduma karibu na wananchi ni njia mojawapo ya kuokoa maisha pale inapotokea dharura kama ambavyo JKCI imesogeza huduma hizo katika Soko Kuu la Kariakoo ambalo hutembelewa na wananchi kutoka nchi mbalimbali.

 Akimuelezea namna huduma zinavyotolewa katika tawi hilo Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rajabu Hamisi alisema tawi hilo limedhamiria kusaidia watu kutoka maeneo mbalimbali wanaopata huduma katika Soko Kuu la Kariakoo.

Rajabu alisema tangu kuanzishwa kwa tawi hilo idadi ya watu wanaotembelea katika kliniki hiyo imekuwa ikiongezeka na kupunguza hadha ya wafanyabiashara kufuata huduma za afya mbali na eneo la biashara.

Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi