Kampeni ya “Jua Namba Zako” yawafikia Mashabiki wa Arsenal
Daktari wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joyce Kyando akimuonesha shabiki wa Timu ya Mpira wa
Miguu ya Arsenal namba tano za afya zinazohimizwa na Wizara ya afya kuzingatia
ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza wakati wa tukio la Ongea na Waziri wa
Afya lililofanyika katika halfa ya kufurahia ushindi wa Timu ya Arsenal leo
katika uwanja wa Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mimbo akimpima sukari kwenye damu shabiki
wa Arsenal aliyefika katika banda la JKCI wakati wa tukio la Ongea na Waziri wa
Afya lililofanyika katika halfa ya kufurahia ushindi wa Timu ya Arsenal leo
katika uwanja wa Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Afisa Utafiti wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akimpima urefu na uzito
shabiki wa Arsenal aliyefika katika banda la JKCI wakati wa tukio la Ongea na
Waziri wa Afya lililofanyika katika halfa ya kufurahia ushindi wa Timu ya
Arsenal leo katika uwanja wa Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Na JKCI
********************************************************************************************************
Mashabiki wa Timu ya
Mpira wa Miguu ya Arsenal wapata elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na
kuzijua namba zao za afya wakati wa hafla ya kusherehekea ushindi wa timu hiyo
iliyofanyika leo katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo imefanyika
sambamba na tukio la Ongea na Waziri wa Afya kutoa motisha kwa mashabiki hao
kufanyiwa uchunguzi wa afya, kuhamasisha kampeni ya Jua Namba Zako na kuikumbusha
jamii kuwa na mtindo bora wa maisha.
Akizungumza wakati wa
halfa hiyo Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joyce Kyando
alisema JKCI itaendelea kuihamasisha jamii kuzifahamu namba zao za afya na
kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.
“Tunaamini mashabiki
hawa wa Arsenal wakishazijua namba zao kupitia hafla hii watajenga tabia ya
kupima afya mara kwa mara na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya
moyo”,
“Unaweza kumuona mtu
anafanya mazoezi kila siku lakini bado akawa na mafuta mengi kwenye damu, hivyo
tusiangalie muonekano wa nje tukajiona salama, tupende kufanya uchunguzi wa
afya”, alisema Dkt. Joyce
Kwa upande wao
mashabiki wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Arsenal walioshiriki hafla hiyo wameishukuru
Wizara ya Afya kuiwezesha JKCI kufikisha huduma za uchunguzi wa afya kwa
mashabiki hao.
Da hope shabiki wa Timu
ya Mpira wa Miguu ya Arsenal alisema wakati mashabiki wa timu hiyo wanapata
burudani pia wamepata nafasi ya kufanya uchunguzi wa afya na ushauri kutoka kwa
wataalamu mabingwa wa magonjwa ya moyo.
Naye Gideon Rwegelela
shabiki wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Arsenal alisema kupitia hafla hiyo watanzania
wengi wataelimika na kuzifahamu namba zao ambazo Wizara ya Afya imekuwa ikihimiza
jamii kuzijua na kuchukua hatua.
Comments
Post a Comment