Posts

Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kuwa na bima ya afya ambayo itawasaidia pindi watakapouguwa

Image
Wataalamu wa magonjwa wa moyo wakiangalia maendeleo ya aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. Lucas Lumambo Selelii aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rosemary Mpella akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. Lucas Lumambo Selelii aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa kufanya hivyo watatambua kama wana maradhi au la na kama wana maradhi wataweza kupata huduma za matibabu kwa wakati. Pia wameombwa kuwa na bima ya afya ambazo zitawasaidia kupata matibabu pindi watakapouguwa kwani maradhi huja muda wowote, wakati wowote na mahala popote bila ya kupiga hodi. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. L...

Shiriki CRDB Bank Marathon kwa ajili ya kuchangisha fedha za matibabu ya moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza kuhusu asilimia kubwa ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo kusumbuliwa na  magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliohusu mbio za CRDB Bank Marathon. Viongozi wa Taasisi mbalimbali ambazo zitashiriki katika mbio za CRDB Bank Marathon wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB   Abdulmajid  Nsekela mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari uliohusu mbio hizo ambazo lengo lake ni  kuchangisha fedha za matibabu ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Viongozi wa Taasisi mbalimbali ambazo zitashiriki katika mbio za CRDB Bank Marathon wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari uliohusu mbio hizo ambazo lengo lake ni ...

WATAALAM WABOBEZI WA MOYO WAPANDIKIZA KIFAA CHA KUUSAIDIA MOYO KUFANYA KAZI VIZURI BILA KUTUMIA MTAMBO WA CATHLAB

Image
Kwa mara ya kwanza wataalamu wabobezi wa moyo na wazibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepandikiza kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Pacemaker) nje ya Taasisi hiyo bila ya kutumia mtambo wa Cathlab. Mgonjwa aliyewekewa pacemaker alipata ajali iliyosababisha uti wa mgongo  kupata shida na kusababisha baadhi ya viungo vya mwili kupoteza  uwezo wa kufanya kazi ikiwemo mishipa ya damu  inayoratibu uwezo wa moyo kutengeneza mapigo yake (Sympathetic Waves System). Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaama daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Yona Gandye alisema kutoka na tatizo alilolipata mgonjwa mara baada ya kupata ajali  mapigo ya moyo yalishuka hadi kufikia 30 kwa dakika na mgonjwa kuonesha   dalili za ukosefu wa mahitaji muhimu ya mwili  yanayosambazwa na mapigo ya moyo ambayo  ni oxygen , ...

*Watanzania washauriwa kulinda afya zao kufurahia ‘matunda’ Uchumi wa Kati*

Image
KULINDA afya kwa kuzingatia mtindo bora wa maisha, ulaji unaofaa, kufanya mazoezi, kuchunguza afya mara kwa mara na kuepukana na mtindo usiofaa wa maisha, ni siri pekee itakayowawezesha Watanzania kufurahia ‘matunda’ Tanzania kuingia nchi zenye Uchumi wa Kati. Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni  na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi alipozungumza na waandishi wa habari , katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA) na kusisitiza kwamba ni wajibu wa kila mmoja kuendelea kulinda afya yake. “Nilipoona nchi yetu imeingia Uchumi wa Kati, nilifurahia sana lakini baadae nikakaa na  kujiuliza, maana yake ni kwamba wananchi watakuwa na hela nyingi zaidi na wataishi maisha marefu zaidi. “Inabidi kama nchi tuanze kuwatayarisha sasa hivi kwa kuwaelimisha jinsi ya kuishi maisha bora wakiwa na afya bora, kwa sababu kwa kutokufanya hivyo, tutajikuta wananchi watakuwa na hela nyingi lakini wakazit...

Nafasi ya mwanamke katika magonjwa ya moyo

Image

MFANYAKAZI BORA ROBO YA NNE YA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 APONGEZWA

Image
Mfanyakazi bora robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 Dkt. Smita Bhalia akipokea Tuzo ya mfanyakazi bora kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumpongeza leo Jijini Dar es Salaam

BILIONEA SANINIU LAIZER ATEMBELEA BANDA LA JKCI NA KUVUTIWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA BANDA HILO

Image
Mtaalam wa maabara kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimweleza Bilionea Saniniu Laizer namna ambavyo maabara ndogo iliyopo katika banda la JKCI inavyotoa huduma ya kuchunguza vipimo vya damu vilivyotolewa kwa wananchi wanaotembelea banda hilo alipotembelea banda la JKCI wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimwelezea Bilionea Saniniu Laizer namna ambavyo wananchi wamekua na mwitikio mkubwa wa kufanya uchunguzi wa afya ya moyo katika banda la JKCI alipotembelea banda hilo kuona huduma zinazotolewa wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam. Bilionea Saniniu Laizer aipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa huduma za ushauri na upimaji wa magonjwa ya moyo wanazozitoa kwa wananchi wanaotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Sal...