Posts

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Kaspar Mmuya atembelea banda la JKCI katika mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Image
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Kaspar Mmuya akizungumza kuhusu umuhimu wa kutoa elimu kwa umma ya magonjwa ya moyo alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza unaofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Malaika jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akiwaeleza baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Mwanza kuhusu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza unaofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lawrence Madole maarufu kama Marlaw akiwasikiliza Daktari Janeth Mmari na Afisa Muuguzi Tunzo Mcharo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimwelezea kuhusu madhara ya mshipa wa damu wa moyo ku...

JKCI kushirikiana na Poland kutibu magonjwa ya moyo

Image

Wanafunzi wa shule ya awali na msingi Libermann watoa msaada

Image
Wahitimu wa darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi ya Libermann wakimkabidhi moja ya zawadi mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Pili Mwinyimkuu ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule ya msingi leo katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi ya Libermann wakimkabidhi moja ya zawadi mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Neema Ryoba ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii baada ya kumaliza salama shule ya msingi leo katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa darasa la saba 2022 shule ya awali na msingi ya Libermann wakimkabidhi msimamizi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambaye pia ni Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Steven Lugu zawadi kwa ajili ya watoto ...

JKCI kushirikiana na Poland kutibu magonjwa ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland Prof. Bartlomiej Guzik wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano katika kutoa huduma za kibingwa na matibabu ya upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland Prof. Bartlomiej Guzik wakitia saini katika mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma za kibingwa za matibabu na upasuaji wa moyo kwa wagonjwa jana Jijini Dar es Salaam   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwaeleza wataalam wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland kuhusu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa JKCI kabla ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma za kibingwa za matibabu na upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo. Picha na: Khamis ...

“Watakaotoa kauli mbaya kwa wagonjwa kuchukuliwa hatua kali”

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi wa Taasisi hiyo wakati wa kufungua mafunzo ya siku mbili ya uadilifu kwa viongozi wa JKCI jana katika ukumbi waTaasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo ya siku mbili ya uadilifu kwa viongozi wa Taasisi hiyo yaliyofanyika jana katika ukumbi wa JKCI uliopo jijini Dar es Salaam. Afisa uchunguzi kutoka Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Grace Kwambiana akiwafundisha viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) maadili ya watumishi wa umma wakati wa mafunzo ya uadilifu kwa viongozi wa Taasisi hiyo yaliyofanyika jana katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo  jijini Dar es Salaam. Picha na: Khamis Mussa  ************************************************************************************************************** Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo J...

Msomali aishukuru JKCI kwa upasuaji wa mtoto wake

Image
  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto Evelyn Furumbe na  Afisa Muuguzi Mariam Makapu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimuhudumia mtoto kutoka nchini Somalia ambaye amefanyiwa upasuaji wa kuzibwa tundu la moyo katika Taasisi hiyo ambaye ameruhusiwa kutoka wodini leo tarehe 07/11/2022. Kulia ni bibi wa mtoto huyo Halimo Isse.  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto Evelyn Furumbe na Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mariam Makapu wakimuhudumia mtoto kutoka nchini Somalia ambaye alifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na kuzibwa tundu la moyo katika Taasisi hiyo, mtoto huyo     ameruhusiwa     kutoka wodini leo tarehe 07/11/2022. Hirs Ally ambaye ni baba mdogo wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kutoka nchini Somalia akimtazama kwa furaha mtoto huyo mara baada ya kuruhusiwa kutoka wodini katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa anapatiwa matibabu. **************************************...

Jumla ya watu 502 wafanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo Mkoani Geita

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kufunga kambi maalum ya matibabu ya moyo iliyokua ikifanywa na wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na wenzao wa CZRH. Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Geita wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi wakati wa kufunga kambi maalum ya matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato CZRH na kumalizika kumalizika hivi karibuni kwa kuwafanyia uchunguzi na matibabu wananchi 502. Baadhi ya wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi wakati wa kufunga kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyokua ikifanywa na wata...