JKCI yapata tuzo utoaji huduma bora za Afya 2025 ngazi ya hospitali maalum na Taifa
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi tuzo ya mshindi wa utoaji wa huduma bora za Afya mwaka 2025 kundi la Hospitali maalumu na Taifa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa maadhimisho ya wiki ya Afya Kitaifa iliyohitimishwa leo jijini Dodoma. Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na mtoto Naima Kasiki aliyewahi kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Afya Kitaifa yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuelezea Waziri wa Afya huduma za utalii tiba zinazofanywa na Taasisi hiyo alipotembelea banda la JKCI wakati wa maadhimisho ya wiki ya Afya Kitaifa yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma Wananchi wa mkoa wa Dodoma wakipata elimu kuhusu magonjwa ya moyo kutoka kwa wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea banda la Taasisi...