Posts

Showing posts from November, 2022

Watoto 22 wafanyiwa upasuaji wa moyo ndani ya siku sita

Image
Wataalam wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel wakifanya upasuaji wa bila kufunua kifua   kwa kutumia mtambo wa Cathlab kuziba tundu la moyo wa mtoto katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi hiyo ambapo jumla ya watoto 22 walifanyiwa upasuaji.  Wataalam wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel wakiangalia tundu la moyo wa mtoto kama limeziba vizuri kwa kutumia mashine ya ECHO wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita iliyomalizika hivi karibu jijini Dar es Salaam. Na: JKCI  ************************************************************************************************************************* Watoto 22 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya dam

Kanali Abas: Kateni bima za afya kuwa na uhakika wa matibabu

Image
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas akuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Mtwara waliofika katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini (SZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tatu inayofanywa na Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa SZRH. Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimsikiliza mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini (SZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tatu inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa SZRH. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Baraka Ndelwa akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini (SZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya si

UZINDUZI WA KAMPENI YA TEMBEA NA JKCI LINDA MOYO WAKO

Image
Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mahali ambapo uzinduzi wa kampeni ya Tembea na JKCI linda moyo wako utafanyika ****************************************************************************************************************************** TAARIFA KWA UMMA   UZINDUZI WA KAMPENI YA TEMBEA NA JKCI LINDA MOYO WAKO Katika utekelezaji wa mpango wa taifa wa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  itazindua  matembezi ya kilomita tano (5KM) kwa ajili ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi duniani. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 02/12/2022 majira ya saa 10 jioni katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Upanga jijini Dar es Salaam. Baada ya uzinduzi kutakuwa na  matembezi ya umbali wa kilomita tano (5KM) yatakayoanzia JKCI kupita mitaa ya Kalenga, Barabara za Umoja wa Mataifa, Bibi Titi, Magore, Malick na kuishia JKCI. Tunawaomb

Kuwait, JKCI kuimarisha matibabu ya moyo kwa watoto

Image

Kwa mara ya kwanza madaktari wazawa wa JKCI wafanya upasuaji wa kubadilisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta)

Image
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akimuelekeza mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kubadilisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao unatoka kwenye moyo mpaka sehemu inayotoa matawi ya mishipa inayopeleka damu kwenye kichwa na ubongo (ascending aorta and arch) Mohamed Dinya kufanya zoezi la kupuliza mashine ijulikanayo kwa jina la Spirometer kwa ajili ya kupanua mapafu baada ya kufanyiwa upasuaji huo ************************************************************************************************** Madaktari wazawa mabingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kubadilisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao unatoka kwenye moyo mpaka sehemu inayotoa matawi ya mishipa inayopeleka damu kwenye kichwa na ubongo (ascending aorta and arch). Upasuaji huo unaojulikana kwa jina la kitaalamu la Bental Procedure and hemi-arch aortic

Kuwait, JKCI kuimarisha matibabu ya moyo kwa watoto

Image
  Daktari bingwa wa usingizi kutoka Shirika linalotoa msaada wa matibabu ya moyo kwa watoto la Children’s Heart Charity Association lililopo nchini Kuwait Hesham Menshawy akielezea namna ambavyo shirika hilo litashirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto walipotembelea JKCI leo jijini Dar es Salaam. Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na mwenzao kutoka Shirika linalotoa msaada wa matibabu ya moyo kwa watoto la Children’s Heart Charity Association lililopo nchini Kuwait Dkt. Faisal Al-Saiedi kuangalia picha ya tundu lililopo kwenye moyo kwa kutumia mashine ya Trans esophageal ECHO kwa mtoto ambaye anarudiwa upasuaji wa moyo wa kuziba tundu na valvu inayovuja walipotembelea JKCI kwa kuangalia namna ya   kushirikiana na Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.  Daktari bingwa wa Upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiwaelezea aina ya upasuaji w

Upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo katika mikoa ya Mtwara na Lindi

Image
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulwa Richard akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya siku tano iliyofanyika mwezi wa Oktoba katika Hospitali hiyo. *********************************************************************************************************************************************************************************   TAARIFA KWA UMMA   UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara pamoja na  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine   watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima. Mkoani Mtwara upimaji utafanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Novemba, 2022 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa

JKCI yaanzisha kliniki ya maumivu ya kifua

Image
  Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo Upanga Jijini Dar es Salaam ambapo huduma zote za matibabu ya moyo zinatolewa. *************************************************************************************************************************************************************************************************************************************** Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha kliniki ya matibabu ya maumivu ya kifua kwa wagonjwa wenye   maumivu ya vichomi kifuani na kifua kubana ili waweze kufanyiwa uchunguzi wa haraka kwani maumivu hayo huambatana na magonjwa mbalimbali ya moyo ikiwemo shambulio la moyo. Akizungumzia leo kuhusu kliniki hiyo inayofanyika JKCI iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo wa Taasisi hiyo Dkt. Tatizo Waane alisema kuwepo kwa huduma hiyo kutawafanya wagonjwa kupata huduma ya matibabu mapema. Dkt. Waane ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema maumivu ya kifua yamekuwepo katika jami

JKCI yaja na kampeni ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kujikinga na magonjwa ya moyo

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea leo jijini Dar es Salaam maT- shirt mawili kati ya 100 kutoka kwa Meneja mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya K4S Security Kemmy David zitakazotumika wakati wa matembezi ya Km.5 kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo. Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Ulinzi ya K4S Security Joseph Goliama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge leo jijini Dar es Salaam baadhi ya maT-shirt kati ya 100 yaliyotolewa na Kampuni hiyo zitakazotumika wakati wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Kampuni ya Ulinzi ya K4S Security walipotembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kumkabidhi T-shirt 100 ambazo zitakaz

JKCI yaokoa milioni 180 matibabu ya wagonjwa 12 nje ya nchi

Image
Wataalam mabingwa wa moyo na matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri wakimfanyia upasuaji wa tundu dogo mgonjwa ambaye mfumo wake wa umeme wa moyo una hitilafu wakati wa kambi maalum ya siku mbili ya matibabu hayo iliyomalizkika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya wagonjwa 12 wenye matatizo ya hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo wametibiwa katika kambi hiyo. *********************************************************************************************************************************************************************** Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa zaidi ya shilingi milioni 180 ambazo zingetumiwa na Serikali iwapo ingewapeleka   wagonjwa 12 wenye hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo (Atrial Fibrillation) kutibiwa nje ya nchi. Wagonjwa hao waliokuwa   na tatizo la uzalishaji wa umeme wa moyo kwa muda mrefu uliosababisha chemba mbili za moyo kufanya kazi bila maw

Kliniki ya maumivu ya kifua yaanzishwa JKCI

Image

Wanachama wa kikundi cha Women Supporting Women watoa msaada kwa watoto

Image
Wanachama wa kikundi cha kusaidiana kiuchumi cha Women Supporting Women wakimkabidhi zawadi mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Yusra Kanyerere wakati wanachama wa kikundi hicho walipowatembelea watoto hao na kuwapa zawadi Wanachama wa kikundi cha kusaidiana kiuchumi cha Women Supporting Women wakimkabidhi zawadi mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Dinna Mrindi wakati wanachama wa kikundi hicho walipowatembelea watoto hao na kuwapa zawadi  Mwenyekiti wa kikundi cha kusaidiana kiuchumi cha Women Supporting Women Ena Mwangama akimkabidhi simamizi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Grace Sanga zawadi zilizotolewa na wanakikundi hao kwa ajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)    Mwananchama wa Kikundi cha kusaidiana kiuchumi cha Women Supporting Women Jacqueline Nshunju akimpatia zawadi mam

Wananchi 50,000 kupata huduma za kibingwa za moyo kwa kufuatwa mahali walipo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari za Afya Aveline Kitomari kutoka gazeti la HabariLeo na James Kandoya wa gazeti la The Guardian kuhusu matokeo ya upimaji wa magonjwa ya moyo uliofanywa na Taasisi hiyo mkoani Arusha wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliomalizika jana jijini Mwanza.   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo akimkabidhi Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari tuzo ya utafiti bora alioufanya kuhusu teknolojia na mbinu za ubunifu za kuzuia na kutibu magonjwa yasiyoambukiza wakati wa mkutano wa nne wa kisayansi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliomalizika jana katika   Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akijibu maswali kuhusu utafiti uliofanywa na Taasisi hiyo kuhusu magonjwa ya moyo na uelewa wa sababu hatarishi za magonjwa hay