Tanzania ya kwanza Afrika kutumia Mashine ya kufuatilia wagonjwa nyumbani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila mashine ya Dozee iliyotengenezwa na Sakaar Health Tech LTD ambayo inatumika kuwafuatilia wagonjwa wa moyo wakiwa nyumbani ili kujua hali zao na kutoa msaada wa haraka endapo utahitajika. *********************************************************************************************************************************************************************************** Kwa mara ya kwanza barani Afrika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Sakaar Health Tech LTD wamezindua rasmi mashine maalum itakayotumika kufuatilia wagonjwa wa moyo wakiwa nyumbani ili kujua hali zao na kutoa msaada wa haraka endapo utahitajika. Kufuatia uzindunzi wa mashine hiyo iitwayo Dozee Tanzania sasa imekuwa nchi ya tatu Duniani kutoa huduma hivyo huku ikiwa nchi ya kwanza barani Afrika. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana jijini Dar es Salaam,mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila ...