Sierra Leone wajifunza JKCI walivyopiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra Leonne huduma zinazotolewa katika kliniki na wodi za watu maalumu na wagonjwa kutoka nje ya nchi wakati walipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dkt. Sartie Mohamed Kenneth akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya wajumbe kutoka nchini humo ambao walitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Msimamizi wa wodi ya watoto ya Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Uuguzi Theresia Tarimo akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra Leonne huduma wanazozipata
watoto waliolazwa katika wodi hiyo wakati wageni hao walitembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika
matibabu ya moyo barani Afrika.
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka nchini Sierra Leonne na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) mara baada ya kumaliza ziara yao ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema matunda ya ziara hiyo ni kuvutia utalii tiba.
"Wenzetu wamekuja kujifunza namna ambavyo tumepiga hatua na tumewaeleza namna Serikali ilivyoamua kuwekeza kwenye matibabu kwa kuajiri wataalamu na kununua vifaa, pia wamejifunza kuanza kuleta wagonjwa hapa nchini kutokana na ambavyo wameona huduma zinavyotolewa na hii ni sehemu ya utalii tiba”, alisema Dkt. Kisenge.
Naye Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI Dkt. Delilah Kimambo alisema matibabu ya moyo si ya daktari peke yake bali ni ushirikiano wa wataalamu mbalimbali hivyo aliwaeleza wataalamu kutoka Sierra Leone ushirikiano wa wataalamu kwenye taasisi hiyo ndiyo kiungo muhimu kwa usalama wa wagonjwa.
Ziara hiyo ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya nchini Sierra Leone ilikuwa ni ya kujifunza namna JKCI ilivyopiga hatua na mbinu walizotumia kwa lengo la kwenda kutumia mbinu hizo kuanzisha taasisi kama hiyo nchini humo.
Comments
Post a Comment