Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa: Fanyeni mazoezi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika matembezi ya pamoja yaliyozinduliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza
matembezi ya pamoja aliyoyazindua leo kwaajili ya kupambana na magonjwa
yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea
daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea
Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja
yaliyozinduliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi
hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano
ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi
Coco beach.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kushiriki katika mazoezi ya pamoja aliyoyazindua rasmi leo kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi waliojitokeza kushiriki mazoezi ya pamoja yaliyozinduliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi ya pamoja yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach.
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akielezea umuhimu wa kufanya mazoezi wakati
wa uzinduzi wa mazoezi ya pamoja kupambana na magonjwa yasiyoambukiza
uliofanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa leo katika viwanja vya Coco beach.
Na: JKCI
**********************************************************************************************************
Wananchi wametakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali
kushiriki katika mazoezi ya pamoja kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
Rai hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akizindua mazoezi ya pamoja
yaliyofanyika katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kassim Majaliwa alisema wananchi wanatakiwa kutenga siku
angalau moja kila wiki kufanya mazoezi ili kupunguza changamoto za magonjwa
yasiyoambukiza.
“Mazoezi haya ya pamoja ambayo nimeyazindua rasmi leo hapa
Dar es Salaam yatafanyika nchi nzima ikiwa ni mkakati wa kupunguza magonjwa
yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya shinikizo la damu, sukari na msongo wa
mawazo”, alisema Mhe. Kassim Majaliwa
Mhe. Kassim Majaliwa alisema kuanzia leo barabara inayotoka
Coco beach kuelekea daraja la tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali
ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road itakuwa ikifunga kila siku ya
jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tatu asubuhi kuwapa nafasi watu wa Dar
es Salaam kufanya mazoezi bila ya kuwa na msongamano wa magari.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alisema kumekuwa
na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza hivyo kama wizara ya afya
inatekeleza wajibu wake mkuu wa kuwakinga watanzania na magonjwa hayo.
“Mwaka 2016 hadi 2019
wakati nawasilisha bajeti ya wizara ya afya kati ya magonjwa kumi
yanayowasumbua watanzania hakukuwa na ugonjwa hata mmoja wa magonjwa
yasiyoambukiza lakini hadi kufikia mwaka 2021 magonjwa hayo yameongezeka kwa
kasi hivyo kuingizwa katika bajeti ya wizara ya afya”, alisema Mhe. Ummy
Mhe. Ummy alisema mazoezi yanasaidia kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza ususani magonjwa ya shinikizo la juu la damu na kisukari kwa
zaidi ya asilimia hamsini.
“Wizara ya afya pamoja na kuweka nguvu kwenye kujenga
hospitali na kununua dawa tutaweka nguvu kwaajili ya kuwakinga watanzania
wasipate magonjwa yasiyoambukiza kwa kuhamasisha mazoezi na mtindo bora wa
maisha”, alisema Mhe. Ummy
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge Kaimu Mkuu wa Hospitali ya JKCI
Dar Group Dkt. Tulizo Shemu alisema kufanya mazoezi kunamsaidia mtu kupunguza
kiwango kikubwa cha rehemu katika mwili.
“Kila dadika kumekuwa kukitokea vifo kutokana na matatizo ya
magonjwa yasiyoambukiza hivyo kwakufanya mazoezi kunapunguza athari za kuweza
kupoteza maisha kutokana na magonjwa hayo”, alisema Dkt. Shemu
Dkt. Shemu alisema tafiti zilizofanyika hivi karibuni
zinaonyesha kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam watu wazima watano hadi sita
kati ya watu 10 wana shinikizo la juu la damu ambapo wagonjwa wengi wanapata
shinikizo la damu kutokana na mtindo wa maisha na kuwa na rehemu nyingi.
“Tukiwa na taratibu za kufanya mazoezi mara kwa mara tutakuwa
tumeweza kupunguza kiwango kikubwa cha magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo
magonjwa ya moyo na kuongeza nguvu kazi katika nchi yetu”, alisema Dkt. Shemu
Comments
Post a Comment