Wauguzi wafundishwa jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi


Daktari bingwa wa wagonjwa wa dharura na mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akiwafundishwa namna ya kumhudumia mgonjwa anayehitaji uangalizi maalumu wauguzi wanaochukua mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa hao yanayotolewa na taasisi hiyo kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Wauguzi kutoka nchini Zambia na mmoja kutoka nchini Tanzania wanaochukua mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakiwa katika mazoezi ya kutumia mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumua (Ventilator).


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akiwafundisha wauguzi wanaochukua mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kumhudumia mtoto aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu wakati wa mafunzo kwa vitendo.

Wauguzi wanaochukua mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakifanya mafunzo kwa vitendo ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

Picha na: JKCI

**********************************************************************************************************


 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)